
Mchana wa leo muda wa saa tisa na nusu Mikoa ya Kanda ya ziwa imekumbwa na tetemeko la ardhi ambapo nyumba kadhaa zimebomoka na kusababisha vifo katika mkoa wa Kagera ambavyo mpaka sasa idadi ya watu kumi (10) wanaripotiwa kupoteza maisha.Katika wilaya ya Karagwe imeripootiwa kifo cha mtu mmoja na nyumba 10 kubomoka huku katika mkoa wa mwanza hakuna vifo wala uharibifu uliotokea japo kulitokea taharuki kubwa watu wakikimbia huku na huku mitaani wakijaribu kuokoa maisha yao.Taarifa kamili ya vifo katika mkoa wa Kagera fuatilia tutakujuza muda wowote mara kamanda wa polisi mkoa wa Kagera atakapotoa taarifa rasmi.