test

Alhamisi, 22 Septemba 2016

TCRA Yadai Haipendi Kufungia vyombo vya Habari ila Sheria Inawalazimu



Mamlaka ya Mawasiliano ya Tanzania, TCRA, imesema haifurahii kuvifungia vyombo vya habari bali inavitaka vifuate kanuni na sheria zilizopo.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui ya TCRA, Joseph Mapunda, ameyasema hayo akiwa jijini Mbeya.

“Hatufurahii vyombo kufungwa, hatufurahii vyombo kupewa adhabu,lengo kubwa ni kuvifanya vyombo viwajibike, kwa mujibu wa sheria viwajibike pia kwa wananchi,viwajibike kwa nchi,” alisema.

“Tunasajili vyombo vingi ili viweze kusaidia, kuhamasisha, kuelimisha, na kuhabarisha wananchi sasa litakuwa halina maana,” aliongeza.

Hivi karibuni kamati hiyo ilikifungia kwa miezi mitatu kituo cha redio cha Radio 5.

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx