test

Jumamosi, 10 Septemba 2016

RAIS MAGUFULI ATEUA MAKATIBU TAWALA WA MIKOA YA RUKWA NA MARA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli jana tarehe 09 Septemba, 2016 amemteua Bw. Ado Steven Mapunda kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara. 

Bw. Ado Steven Mapunda anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Benedict Richard Ole Kuyan ambaye amestaafu. 

Pia, Rais Magufuli amemteua Bw. Tixon Tuliangine Nzunda kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa. 

Bw. Tixon Tuliangine Nzunda anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Symthies Emmanuel Pangisa ambaye amestaafu. 

Tarehe ya kuapishwa kwa Makatibu Tawala wa Mikoa walioteuliwa itatangazwa baadaye. 


Gerson Msigwa 
Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU 
Dar es Salaam 
09 Septemba, 2016

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx