Siku moja baada ya kuibuka washindi wa kombe la CECAFA Woman Challenge, timu ya wanawake ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Queens imewasili nchini kwa kupitia mkoani Kagera ambapo Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Generali Mstaafu Salim Kijuu amewapokea.
Jungukuu leo imekuandalia picha jinsi Kili Queens ilivyowasili Kagera.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Generali Mstaafu Salim Kijuu akisalimiana na baadhi ya wachezaji wa Kilimanjaro mara baada ya kuwasilini Mkoani Kagera wakitokea nchini Uganda kushiriki mashindano ya CECAFA kwa wanawake ambapo wameibuka mabingwa kwa mwaka 2016.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja, Generali Mstaafu Salim Kijuu akipokea kikombe cha ubingwa wa CECAFA kwa wanawake kutoka kwa Nahodha wa Kilimanjaro Queens, Sophia Mwasikili.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Generali Mstaafu Salim Kijuu(kushoto) akiinua juu kikombe cha ubingwa wa CECAFA kwa wanawake alichokipokea kutoka kwa Nahodha wa Kilimanjaro Queens Sophia Mwasikili(kulia).
Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Generali Mstaafu Salim Kijuu(kushoto) akipokea Bendera ya Taifa kutoka kwa katibu wa Chama cha Mpira mkoani Kagera Bw. Salum Chama mara baada ya Mabingwa wa CECAFA kwa wanawake Kilimanjaro Queens kuwasili kutoka Nchini Uganda katikati ni Mwenyekiti wa Soka la wanawake Amina Karuma.