test

Jumamosi, 10 Septemba 2016

Nyota 9 wa kuwatazama wikiendi hii Ligi Kuu England


LONDON, England
BAADA ya ligi kubwa kusimama sehemu mbalimbali duniani ili kupisha  michuano ya timu za taifa wiki iliyopita, utamu wa ligi hizo umerudi hususani ligi pendwa England inayotajwa kutazamwa na idadi kubwa ya watu ulimwenguni kote inaanza tena.
Ligi hiyo itakuwa na wachezaji kadhaa wapya vikosini wakiwa na klabu mpya wakiwemo ambao uhamisho wao ulifanyika dakika za lala salama dirisha hilo la majira ya kiangazi kufungwa.

Hawa ni baadhi ya mastaa kadhaa wanaotazamiwa kufanya vizuri kwenye klabu zao hizo mpya huku wakifuatiliwa kwa karibu na mashabiki wao miongoni mwao akiwemo, Jack Wilshere,  aliyepelekwa kwa mkopo Bournemouth  akitokea Arsenal.
Shkodran Mustafi (Arsenal)
Beki wa kati alisajiliwa na kocha Arsene Wenger kwa pauni milioni 25 akitokea Valencia ya Hispania, saa chache kabla ya dirisha la usajili kufungwa.
Mjerumani huyo amerejea kwa mara nyingi katika mikikimikiki ya Ligi Kuu England baada ya kuondoka miaka kadhaa alipokuwa akiitumikia Everton  na kutua Sampdoria kabla ya kutua  Valencia 2014 alipochukuliwa na Arsenal mwaka huu.
Mustafi mshindi wa Kombe la Dunia akiwa na timu yake ya Ujerumani 2014 nchini Brazil, ametua Arsenal kutengeneza ukuta mgumu akicheza sambamba na Laurent Koscielny, kutokana na Per Mertesacker kusumbuliwa na majeruhi.
Mustafi anatajwa kuingia kwenye kikosi cha kwanza moja kwa moja kuchukua nafasi ya Rob Holding, ambaye mechi zake za awali alilipwa kiasi chake na kushindwa kutengeneza kombinesheni ya kuridhisha kati yake na Koscielny.
Jack Wilshere (Bournemouth)
Raia wa England kipenzi cha mashabiki washika mitutu wa London, Arsenal aliyetolewa kwa mkopo  dakika za mwisho kabisa za uhamisho kwenda kukipiga katika klabu ya Bounermouth.
Wilshere mwenye umri wa miaka 24, ameungana na kocha Eddie How  ambaye ni Mwingereza mwenzake, huku akilipwa kiasi cha pauni milioni 100 kwa wiki.
Kiungo huyo mshambuliaji mwenye kipaji kikubwa cha soka, huenda akaanza kikosi cha kwanza jioni ya leo dhidi ya West Brom, ndani ya maisha mapya tofauti na yale ya viunga vya Emirates.
Jeff Hendrick (Burnley)

Kiungo wa timu ya taifa ya Jamhuri ya Ireland aliyeweka rekodi ya klabuni kwake Derby Country ya Daraja la Kwanza ‘Championship’, uhamisho wa  kitita cha fedha nyingi pauni milioni 10 kwenda Burnley
Licha ya kocha wake wa awali katika  klabu ya Derby Pearson kuweka ngumu ya kuondoka kwa nyota wake huyo, lakini Jeff Hendrick mwenyewe hakuwa tayari kutua viunga hivyo vya iPro, alipodumu miaka sita.
Kiungo huyo atakuwa sura mpya  Burnley anayetazamiwa kufanya vyema mahali hapo ikiwemo mechi ya leo dhidi ya Hull City, endapo tu kama atapangwa na kocha wake, Sean Dyche.
David Luiz (Chelsea)

Kocha Antonio Conte alichukua  maamuzi magumu ya kumsajili David Luiz kwa pauni milioni 34 kutoka PSG ya Ufaransa, kutokana na mapungufu ya beki wake wa kati ikiwa ni baada ya miaka miwili tangu kuondoka kwa Mbrazil huyo Stamford Bridge.
Uzoefu wa Luiz na kuifahamu vizuri  ligi hiyo ataongoza ukuta wa Chelsea  sambamba na Gary Cahil aua John Teryy, huku Kurt Zouma anayetajwa  chaguo la kwanza la Conte bado anauguza majeruhi yake.
Hata hivyo, akirejea Zouma, Conte  huenda akawatumia mabeki watatu  nyuma kama ilivyo kwa mfumo wa Kiitalia, ambapo taarifa zinasema nafasi kubwa watepewa kina Luiz, Zouma na beki mwingine mpya, Marcos Alonso.
Islam Slimani (Leicester)

Leicester ambao ni mabingwa watetezi waliweka rekodi ya kusajili washambuliaji wawili msimu huu kwa nyakati tofauti wote wakitoka barani ambapo walianza na Mnaigeria, Ahmed Musa pauni milioni 16.
Na baada ya hapo wakanasa saini ya straika kutoka taifa la Algeria, Islam Slamani, wakiweka mezani kitita cha pauni 29 kumchomoa Sporting Lisbon ya Ureno.
Msimu uliyopita Slimani alifanikiwa kuifungia klabu yake hiyo ya zamani Lisbon mabao 31 hatua iliyompelekea  kuzivutia klabu mbalimbali za Ligi Kuu England na hatimaye akaangukia mikononi mwa Leicester.
Wastani wake huo mkubwa wa kuingia  wavuni utamfanya kocha Claudio Ranieri, kumtumia zaidi kikosini hapo nyuma au mbele ya Jamie Vardy na ingawa wachambuzi wengi wanaamini  ubora ziadi wa Slimani unamfaidi akicheza kama namba tisa, wakati huo mawinga wakiwa ni Shinji Okazaki na Riyad Mahrez.
Ilkay Gundogan (Man City)

Usajili wa awali kabisa tu wa kocha Pep Guardiola alivyotua Etihad, kiungo huyo wa zamani wa Borussia Dortmund  inaelezwa yuko fiti hivi sasa kucheza Manchester Derby.
Gundogan (25) licha ya kukosa michuano kadhaa akiwa Dortmund msimu uliopita ikiwemo Ligi ya Mabingwa kutokana na kuuguza majeraha, lakini sasa mazoezini ameonekana kurudi kwa kasi  kama ilivyokuwa kipindi cha nyuma na kumshawishi zaidi kocha wake kumpa nafasi kikosi cha kwanza.
Mchezo huo wa leo City tayari watamkosa mshambuliaji wao, Sergio Aguero, kutokana na kulimwa adhabu na FA, ikielezwa nafasi yake huendwa ikachukuliwa na kinda Mnaigeria,  Kelechi Iheanacho.
Kama ilivyo falsafa ya Guardiola kutumia viungo wengi wenye uwezo wa kumiliki mpira akitumia mfumo wa 4-1-4-1, itawajumuisha kina David Silva  Kevin de Bruyne, Fernando na Gundogan, mbele akisimama Nolito.

Calum Chambers (Middlesbrough)

Ujio wa Mustafi ndani ya Arsenal na kinda Rob Holding, umemfanya Chambers  kupelekwa kwa mkopo na kocha wake, Arsene Wenger,  Middlesbrough zikiwa zimebaki siku mbele usajili kufika tamati.
Chembers ataungana na wakongwe wengine  mahali hapo kama Adam Clayton na Grant Leadbitter, beki huyo mwenye uwezo kucheza beki wa kati  na kulia kocha wake Karanka  kamuweka kwenye orodha ya kikosi chake kitachopambana leo  na Crystal Palace  yenye mshambuliaji matata Christian Benteke.

Wilfried Bony (Stoke City)

Kocha Mark Hughes amekenua meno  yote nje na kujinadi lazima kumfanya  mshambuliaji wake huyo mpya aliyetokea Manchester City kwa mkopo kung’ara akisaidiana na wakali wengine kama Marko Arnautovic, Bojan na Xherdan Shaqiri.
Bony raia wa Ivory Coast, inaelezwa ameshindwa kutengeneza kombinesheni nzuri kati yake na Sergio Aguero na kudorora kabisa Etihad tofauti na alivyokuwa bora katika klabu ya Swansea City.
Akifanikiwa kufunga jumla ya mabao 35 akicheza mechi 70, anatarajiwa kuwepo leo dimbani Bet365 kuwapa kashikashi mabeki wa Tottenham  ambao watakuwa wageni wa mchezo huo.

Moussa Sissoko (Tottenham)

Nyota mwingine aliyesajiliwa dakika za mwisho kufungwa kwa dirisha la usajili Agosti 31 akisafiri kwa ndege binafsi kutoka Newcastle hadi London ndani ya klabu ya Tottenham.
Dili lilifanywa na Tottenham kwa kuwapokonya tonge mdomoni Everton ambao walikuwa nao kwenye hatua za mwisho kumalizana na Mfaransa kumsubiri viunga vya Goodison Park, lakini akaamua kwenda White Hart Lane.
Sissoko alimvutia zaidi kocha Mauricio Pochettino, baada ya kuonyesha  kiwango cha juu kwenye timu yake ya taifa ya Ufaransa katika michuano ya Euro 2016.

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx