Kwenye
picha Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, George Simbachawene
akisalimiana na meneja wa NMB tawi la Musoma, Sebastian Kayanga
alipokuwa anaingia kwenye ukumbi wa Mikutano wa Mwembeni Complex kwa
ajili ya ufunguzi rasmi wa Mkutano wa mwaka wa ALAT Taifa. NMB
imedhamini mkutano wa ALAT Taifa kwa shilingi Milioni 206 ikiwa ni
gharama za mkutano na zawadi kwa ajili ya Meya bora wa Mwaka. Pichani
kulia ni Kaimu Meneja wa NMB Kanda ya ziwa, Amos Mubusi.
Kupitia
mkutano huo NMB imeelezea jinsi ilivyounganisha mfumo wake wa kibenki
na mfumo wa serikali za mitaa (LGRCIS) kufanikisha ukusanyaji mapato ya
kwa wakati na bila kupotea na kuandaa vituo vya makusanyo ya fedha
kusaidia serikali katika makusano.
Akitoa mada kwenye mkutano huo ulioingia siku ya 2 hii leo,Afisa Mkaguzi Mkuu wa ndani wa (NMB) Augustino Mbogella,amesema licha ya kusaidia serikali katika suala zima la ukusanyaji wa mapato, benki hiyo pia imesaidia miradi ya maendeleo ya jamii ikilenga zaidi katika utoaji wa misaada katika sekta ya elimu na afya.

Mbogella
amesema mwaka 2015 pekee zaidi ya shule 140 za msingi na sekondari
zilipata zaidi ya madawati 7,000 kwa Tanzania nzima katika mpango wa
kuendelea kutatua tatizo la madawati mpaka kufikia septemba 2016 tayari
wametumia zaidi ya milioni 900.
“Upande wa afya tumetoa vifaa mbalimbali kwenye hospitali 50 za serikali pamoja na vituo vya afya ambapo kiasi cha fedha takribani shilingi milioni 200 zilitumika” alimalizia Augustino Mbogella.
“Upande wa afya tumetoa vifaa mbalimbali kwenye hospitali 50 za serikali pamoja na vituo vya afya ambapo kiasi cha fedha takribani shilingi milioni 200 zilitumika” alimalizia Augustino Mbogella.
Wakati
huo, viongozi na wananchi wameombwa kutembelea banda la NMB ili kuweza
kupata elimu zaidi likiwemo pia suala la ufunguaji wa akaunti mbambali
kwenye benki hiyo ambazo zina manufaa makubwa.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI) George Simbachawene,akisaini kitabu
cha wageni kwenye banda la NMB kwenye maonyesho ya ALAT.