Ameyasema hayo akiwa mkoani humo lipoambatana na viongozi wa chama hicho huku akisema licha ya jitihada ilizofanywa na serikali na wadau wengine bado kunahitajika msaada zaidi kwa waathiriwa wa tetemeko hilo
“Nawapeni pole, poleni sana, mwenzangu ameeleza kwa kirefu, sio mahali pa malumbano, lakini tunataka haki itendeke, tumekuja na msaada kidogo iko pale mkoani mtaipata, tuna hakika mtapewa misaada mingine kwa watanzania ambao wanajitolea na serikali inajitolea,” alisema.
Lowassa alisema madhara yaliyojitokeza ni makubwa hivyo watanzania wote wanabudi kuwasaidia waathirika wa tetemeko la ardhi.
Hivi karibuni Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Walemavu, Jenista Muhagama akiwa mkoani humo alisisitiza kuwa suala la tetemeko si la serikali peke yake bali ni la watanzania wote.