Gazeti hilo limesema Magufuli ana zaidi ya asilimia 95 ya sifa ambazo kiongozi yoyote yule barani Afrika anahitaji ili kuipeleka nchi yake mbele, huku likisema uwezo wa Magufuli kusimamia utumishi wa umma, kupambana na rushwa uongozi madhubuti ni vitu muhimu sana kwa taifa lolote Afrika.
Pia wameenda mbele sana na kudai nchi yoyote ile barani Afrika inahitaji sana huduma za afya,elimu bora,chakula na uchumi imara kuliko inavyohitaji demokrasia.