Serikali
kupitia Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo imedhamiria
kurasimisha kazi ya sanaa kuwa shughuli rasmi ya kiuchumi katika kipindi
cha miaka mitano ya uongozi wa Rais Dkt.John Pombe Magufuli.
Hayo
yamesemwa na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape
Moses Nnauye alipokuwa akizundua msimu wa tatu wa kipindi cha
televisheni cha kusaka vipaji vya wasanii chipukizi cha Club Raha Leo
Show na kuahidi kutoa ushirikiano kwa wadau wa sanaa na wasanii ili
kufanikisha azma ya serikali ya kurasimisha sekta hiyo kuwa rasmi kama
shughuli ya kiuchumi.
“Tutashirikiana
na nyinyi katika kuiendeleza sekta ya sanaa nchini ili kuwezesha vijana
wengi wenye vipaji kuweza kujiajiri na kuajiri wengine kupitia kazi zao
za sanaa” alisema Mhe. Nape.
Mhe.
Nape Moses Nnauye amewaomba wadau mbalimbali kujitokeza kudhamini
mashindano mbalimbali ya kuibua vipaji vya wasanii chipukizi ili kuweza
kufikia malengo ya kuendeleza sekta ya sanaa nchini.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Dkt
Ayoub Rioba amesema kuwa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC)
litaendelea kushirikiana na wadau wa sanaa nchini kuibua na kuendeleza
vipaji vya wasanii mbalimbali ili kuwezesha sanaa kuwa ajira rasmi
katika kuinua kipato cha msanii na uchumi wa taifa kwa ujumla.
Naye
Mratibu wa Club Raha Leo Show Bibi. Susan Mungi amesisitiza wasanii
kuheshimu kazi zao na kuzifanya kwa ustadi mkubwa kwani ndio nyezo
muhimu katika kuendeleza kazi ya sanaa nchini kwa kuifanya kuwa kazi
mojawapo ya kiuchumi.
Club
Raha Leo Show ilianzishwa kama Kipindi cha redio kilichorushwa Redio
Tanzania Dar es Salaam (RTD) na baadae kuwa shindano kubwa Tanzania la
kusaka, kuibua na kuendeleza vipaji vya wasanii wanaochipukia nchini, na
huu ni msimu wa tatu wa shindano hilo.