Rapper
Nay wa Mitego amedai ametimiza matakwa aliyopewa na Baraza la Sanaa la
Taifa (BASATA) baada ya kufungiwa kwa wimbo wake wa ‘Pale Kati’, ambapo
Jumatano hii taachia version ya kwanza ya video ya wimbo huo.
Nay amewataka mashabiki wake wa muziki wa kimataifa kukaa mkao wa kula.
“Mimi na BASATA tulishamalizana, wao walinipa maazimio na mimi nimeshayatekeleza, kwa hiyo na mimi naendelea na issue zingine,” alisema Nay.
“Jumatano hii mashabiki wangu Wakimataifa pamoja na wa kwenye mitandao ya kijamii wakae mkao wa kula, naachia video,”
Rapper
huyo alisema wimbo wa ‘Pale Kati’ una nguvu kubwa sana na unafanya
vizuri katika baadhi ya nchi kama Kenya, Uganda pamoja na Ghana, na ndio
maana ameamua kuanza kutoa video kwa ajili ya kimataifa kwanza.
Pia amewataka mashabiki wa muziki wake kuendelea kusubiria mambo mazuri kwani wimbo huo una video nne.