WATUMIAJI
wa pombe sasa wataweza kupata auheni ya bei ya vinywaji hivyo, baada ya
wanasayansi kugundua kifaa maalumu kitakachotumika kubadilisha mikojo
ya walevi kutumika kutengenezea bia.
Kugunduliwa
kwa kifaa hicho ni mkombozi kwa wamiliki wa viwanda vya pombe ambapo
wataweza kupata malighafi ya kutengenezea bia kwa urais.
Kinatarajiwa kufungwa kwenye vyoo vya baa mbalimbali ili kurahisisha upatikanaji wa mikojo hiyo ya walevi.
Kifaa hicho ambacho kitakuwa kikitumia umeme wa jua pia kitakuwa na uwezo wa kubadili mikojo hiyo kutumika kama maji ya kunywa.
Timu
ya watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Ghent nchini Ubeligiji, walisema
kifaa hicho kitaanza kutumika hususan maeneo ya mijini kwenye nchi
zinazoendelea.
Licha
ya kuwepo kwa mashine maalum yenye uwezo wa kutibu maji machafu ikiwemo
mkojo kisha kutumika kwa matumizi mengine muhimu ya binaadamu,
wataalamu hao wamesema kifaa hicho walichokigundua kinauwezo zaidi wa
kuyatibu maji hayo bila kutumia nguvu ya umeme.
Dk.
Sebastiaan Derese, alisema kifaa hicho kitakuwa kikitunza mikojo kwenye
tangi maalum ambalo litatumika kutibu kisha kutumika kama malighafi ya
kutengenezea bia.
Kwa
mara ya kwanza kifaa hicho kilianza kutumika kwenye tamasha la muziki
ililofanyika mjini humo ambapo jumla ya lita 1000 za mikojo,
zilikusanywa kisha kutengenezewa bia.
Alibainisha kuwa, bia zilizotengenezwa kupitia mikojo hiyo imewavutia wanywaji wengi hususan kwenye matamasha mbalimbali.