Akikabidhi madawati hayo,meneja mkuu wa mgodi wa Buzwagi Mhandisi Asa Mwaipopo amesema Kampuni yake imekabidhi kiasi hicho cha madawati kwa lengo la kuunga mkono jitihada za mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania Dkt. John Pombe Magufuli kupunguza uhaba wa madawati katika shule za msingi na sekondari.
“Mgodi wa Buzwagi unaunga mkono jitihada zinazofanywa na rais wa awamu ya tano,Dkt. John Pombe Magufuli katika kumaliza tatizo la wanafunzi kukaa chini,tumeamua kutekeleza kwa vitendo jitihada hizo” ,alieleza Mwaipopo.
Akipokea madawati hayo Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Bi Zainab Telack ameupongeza mgodi wa Buzwagi kwa mchango wao uliolenga kuunga mkono jitihada za mheshimiwa rais Magufuli, katika kuhakikisha kuwa watoto wote wanakaa kwenye madawati.
“Nimefarijika sana kuona mnaunga mkono serikali,tulikuwa na upungufu wa madawati lakini kwa msaada huu wa madawati mmesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza tatizo”,alisema Telack.
Aidha Mkuu huyo wa Mkoa wa Shinyanga amewataka wakurugenzi wa halmashauri zote katika mkoa wa Shinyanga kuwachukulia hatua kali za kisheria wazazi wote wanaowaachisha masomo wanafunzi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa Kahama Abeli Shija akishukuru kwa niaba ya halmashauri za mkoa wa Shinyanga, ameupongeza Mgodi wa Buzwagi kwa jitihada zao mbalimbali katika kutekeleza miradi ya kimaendeleo katika mkoa wa Shinyanga na hususani wilaya ya Kahama.
Hafla hiyo ya kukabidhi madawati ilifanyika Julai 28,2016 katika Shule ya Msingi Majengo iliyoko wilayani Kahama katika halmashauri ya mji wa Kahama ambapo ilihudhuriwa pia na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Shinyanga,viongozi wa wilaya ya Kahama,uongozi wa Mgodi wa Buzwagi, walimu na wanafunzi wa shule ya msingi Majengo.


Wanafunzi wa shule ya msingi Majengo iliyopo katika halmashauri ya mji wa Kahama wakipiga makofi kumkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga wakati wa hafla ya kupokea madawati kutoka kwa uongozi wa Mgodi wa Buzwagi.

















Wanafunzi wa shule ya Msingi Majengo wakifurahia mara baada ya shule yao kupokea baadhi ya madawati kutoka kwa uongozi wa Mgodi wa Buzwagi.