test

Jumapili, 13 Septemba 2015

MAMA SAMIA, NAPE NA MAMA SALMA KIKWETE WAITIKISA LINDI MKUTANO WA KAMPENI



 Aliyekuwa Katibu wa wilaya ya Lindi mjini wa Chadema, AbdallaMadebe ambaye alikuwa ndiye mpigadebe mkubwa wa Mbunge anayemaliza mda wake wa Lindi mjini, maarufu kwa jina la Bwege, akibebwa na wananchi baada ya kutangaza kuhamia CCM, katika mkutano wa kampeni uliofanywa na Mgombea wenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan katika eneo la Mnazi Mmoja, mkoani Lindi leo. Pamoja na Katibu huyo wanachama wengine 38 walihamia CCM.
 Wananchi akishangilia wakati wa mkutano wa kampeni uliofanywa na Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan leo katika eneo la Mnazi Mmoja mkoani Lindi
 Katibu wa NEC, Itkadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akimkaribisha jukwaani, Aliyekuwa Katibu wa wilaya ya Lindi mjini wa Chadema, AbdallaMadebe ambaye alikuwa ndiye mpigadebe mkubwa wa Mbunge anayemaliza mda wake wa Lindi mjini, Maarufu kwa jina la Bwege, wakati alipoamua  kutangaza kuhamia CCM, katika mkutano wa kampeni uliofanywa na Mgombea wenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan katika eneo la Mnazi Mmoja, mkoani Lindi leo. Pamoja na Katibu huyo wanachama wengine 38 walihamia CCM.
 Shamrashamra zikirindima wakati Nape akimtangaza Aliyekuwa Katibu wa wilaya ya Lindi mjini wa Chadema, AbdallaMadebe ambaye alikuwa ndiye mpigadebe mkubwa wa Mbunge anayemaliza mda wake wa Lindi mjini, maarufu kwa jina la Bwege baada ya kutangaza kuhamia CCM, katika mkutano wa kampeni uliofanywa na Mgombea wenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan katika eneo la Mnazi Mmoja, mkoani Lindi leo. Pamoja na Katibu huyo wanachama wengine 38 walihamia CCM.
 Mgombea wenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akihutubia mkutano wa kampeni za CCM aliofanya katika eneo la Mnazi Mmoja, mkoani Lindi leo
Mgombea wenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan na Mjumbe wa NEC, Lindi Mjini Mama Salma Kikwete wakiwasalimia wananchi wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika eneo la Mnazi Mmoja, mkoani Lindi
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akimsikiliza kwa makini, aliyekuwa Mpigadebe Mkuu wa CUF, Lindi Mjini, Mohammed Omari baada ya kutangaza kuhamia CCM leo katika mkutano wa kampeni uliofanyika eneo la Mnazi Mmoja mkoani Lindi
 Mke wa Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, Mama Salma Kikwete akihutubia mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika eneo la Mnazi Mmoja mkoani Lindi
 Wananchi wakiwa na bango la kufagilia uamuzi wa CCM kumpatia nafasi mwanamke Mama Samia Suluhu Hassan kuwa Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo eneo la Mnazi Mmoja, mkoani Lindi.
 Mgombea Mwwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akiwa na Mama Salma Kikwete na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Lindi Mzee Mtopa, baada ya kuwasili kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika leo eneo la Mnazi Mmoja mkoani Lindi
 Mgombea Mwwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akijadiliana jambo na Mama Salma Kikwete na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Lindi Mzee Mtopa, baada ya kuwasili kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika leo eneo la Mnazi Mmoja mkoani Lindi
 Wasanii wa Bongo Movie kina Wema Sepetu wakiwa kwenye mkutano wa kampeni uliofanywa na Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan katika eneo la Mnazi Mmoja mkoani Lindi leo
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwasili meza kuu wakati wa mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika leo eneo la Mnazi Mmoja mkoani Lindi leo
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu akiwasili meza Kuu wakati wa mkuano wa kampeni uliofanyika leo katika eneo la Mnazi Mmoja mkoani Lindi
 Msafara wa Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu, ukipokewa na waendesha bodaboda ulipowasili Lindi Mjini leo ukitokea jimbo la Mchinga mkoani Lindi
 Wananchi wakiwa katika shamrashamra wakati wa mkutano wa kampeni uliofanywa na Mgombea Mwenza w Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan katika jimbo la Mchinga mkoani Lindi leo
Mwananchi akiwa na bango la Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, Katika mkutano wa kampeni za CCM uliohutubiwa na Mgombea Mwenza wa Urais Mama samia Suluhu Hassan katika jimbo la Mchinga mkoani Lindi leo
 Mbunge wa zamani wa Mchinga,Muhdhihir Mudhihir akiteta jambo na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Lindi Mzee Mtopa katika mkuano wa kampeni uliofanyika katika jimbo hilo leo
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akishauriana jambo na Mgombea Ubunge jimbo la Mtera Said Mtanda, katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo hilo
 Mbunge wa zamani wa Jimbo la Mchinga, Mudhihir Mudhihir akihutubia katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo hilo mkoani Lindi
 Wananchi wakimsikiliza kwa makini Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama samia Suluhu Hassan katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo la Mchinga mkoani Lindi
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia suluhu Hassan akimnadi mgombea Ubunge jimbo la Mchinga Said Mtanda, wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo hilo mkoani Lindi. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx

0 comments:

Chapisha Maoni