Mgombea
urais kwa tiketi ya chama cha mapinduzi Dr John Pombe Magufuli amesema
serikali ya awamu ya tano atakayoiunda baada ya uchaguzi mkuu wa October
25 iwapo atapata ridhaa ya watanzania, itatoa kipaumbele kwa sekta
binafsi nchini kushiriki katika uchumi wa gesi na mafuta badala ya
wageni ili kuliwezesha taifa kunufaika vya kutosha na sekta hiyo badala
ya kuwachia wageni pekee kwa kuwa hakuna nchi inayoendelea bila
kuwashirikisha wazawa katika maliasili zake lakini pia kuimarisha
bandari ya Mtwara pamoja na ujenzi wa reli kutoka Mtwara mpaka Mbamba
bay.
Kauli hiyo ya Dr Magufuli ameitoa mkoani Mtwara wakati akizungumza
na wakazi hao kwa nia ya kuomba kura ili aweze kuunda serikali ya awamu
ya tano na kuongeza kuwa sekta binafsi nchini ina nafasi kubwa ya
kuliwezesha taifa kupiga hatua za haraka za kimaendeleo iwapo
itashirikishwa vya kutosha katika rasilimali mpya ya mafuta na gesi na
kwamba serikali yake imedhamiria kuishirikisha sekta binfsi na hasa
wazawa katika sekta hiyo.
Aidha Dr Magufuli ameongeza kuwa Tanzania ni nchi tajiri yenye
rasilimali za kutosha na kwamba rasilimali hizo zikitumiwa vyema
zinaweza kulifanya taifa kuwa nchi ya uchumi wa kati na kupunguza
umasikini uliopo hivi sasa miongoni mwa watanzania na kwamba
kinachohitajika na uongozi makini wenye dhamira ya dhati ya kuwatumikia
wananchi na kwamba kazi hiyo inaiweza.
Akitokea wilayani Masasi kuelekea mjini Mtwara Dr Maufuli
amezungumza na watanzania aliokuwa akikutana nao njiani lakini pia
amefanya mikutano katika wilaya ya Newala, Tandahimba, Mtwara vijijini
na baadae Mtwara mjini ambapo mmoja wa wagombea wabunge katika mkoa huo
wa Mtwara amemtaka Dr Magufuli kuhakikisha Mtwara inakuwa na shule
pamoja na vyuo vingi ili kuwawezesha wananchi kunufaika na rasilimali ya
mafuta na gesi.
Dr Magufuli tangu kuanza kwa ziara zake za mikoani kwa ajili ya
kampeni ya kusaka urais ametembea zaidi ya kilomita elfu nne na mia saba
kwa njia ya barabara kwa kile alichosema ni kutaka kujionea mwenyewe
shida za watanzania badala ya kusimuliwa ili akipata ridhaa ya
watanzania aweze kuzitatua.
0 comments:
Chapisha Maoni