Wananchi
wameeleza kuchoshwa na rushwa ambayo wameitaja kama saratani
inayodumaza maendeleo ya nchi na kutaka rais ajaye apambana na tatizo
hilo kwa dhati bila woga .
Wakizungumza
katika mwendelezo wa kampeni za kumnadi mgombea wa kiti cha urais
kupitia CCM Dr.John Pombe Magufuli wananchi hao wa mji wa Meatu
wamesema kukosekana kwa huduma nyingi za kijamii ili kumrahisishia
maisha mtanzania wa kawaida kunasababishwa na vitendo vya rushwa
vinavyofanywa na watendaji wa serikali jambo linaloonekana kama
utaratibu wa kawaida hivyo kumtaka rais ajaye kukomesha vitendo vya
rushwa kwa vitendo katika sekta zote za utoaji wa huduma.
Mgombea
wa kiti cha urais kupitia CCM Dr.John Pombe Magufuli kwa upande wake
ameeleza kuchukizwa na vitendo vya rushwa na ufisadi kunakosababisha
huduma kutomfikia mwananchi wa kawaida na kwamba litakuwa suala la
kipaumbele kupambana nalo na kuwataka watendaji wajipange kutoa huduma
bora na kutatua kero za wananchi.
Aidha
Dr.Magufuli ameongeza kuwa serikali ya awamu ijayo endapo atapata
ridhaa mbali na kutaka uchumi wa nchi uendeshwe kwa kutegemea viwanda
pia atatilia mkazo katika sekta ya uvuvi na kilimo hususani cha mazao
yanayowaingizia kipato kikubwa wananchi ili kukuza kipato cha kaya na
taifa lakini pia kupunguza kiwango cha umasikini nchini.
Mh.Luaga
Mpina akiwawakilisha wananchi wake amemuoba Dr. Magufuli atakapoingia
ikulu kusaidia kutatua kero kubwa inayowakumba wananchi wa meatu ambao
kwa kiasi kikubwa ni wafugaji na wakulima kuwatengea maeneo ya kilimo na
ufugaji ili kupunguza migogoro iliyopo.
Dkt.Magufuli
atahitimisha ziara ya kunadi ilani ya ccm katika wilaya za mkaoa wa
simiyu na kuingia mkoani tabora kuhutubia mkutano wa hadhara wa kuomba
ridhaa kwa watanzania waishio mkoani Tabora.
0 comments:
Chapisha Maoni