Chama cha ACT wazelendo jana kimenza mafunzo ya siku mbili mfululizo kwa wagombea wake wa nafasi za ubunge nchini mafunzo ambayo yamelenga kuwajengea uwezo na kujiamini zaidi kuelekea kufanya kampeni na kutafuta nafasi za uwakilishi wa katika majimbo mbalimbali kikiwa ni chama pekee nchini Tanzania kulichoendesha mafunzo kama hayo kwa sasa.
Kiongozi
mkuu wa chama hicho Zitto Kabwe akizungumza na wanahabari wakati wa
mafunzo hayo alisema kuwa chama hicho ni chama pekee nchini Tanzania
kilichodiriki kuwapa mafunzo ya kuelekea katika uchaguzi ili kuwaweka
katika mstaari mmoja wa kuhakikisha kuwa wanakwenda na lugha moja kwa
watanzania kueleza mipango na ilani ya chama hicho.
Zitto
alisema kuwa chama cha ACT wazalendo ndio chama pekee nchini Tanzania
ambacho kina agenda maalum kwa watanzania tofauti na vyama vingine
ambavyo alisema kuwa vinatumia mbwembwe na ulaghai kwa watanzania bila
kuweka wazi nini wanataka kuwafanyia watanzania.
Alisema
kuwa mambo ambayo chama hicho kimekuwa kikiyapigania na kitaendelea
kuyapigania ni pamoja na mambo ya hifadhi ya jamii kuhakikisha kuwa
watanzania wote wanafaidika nayo,pamoja na miiko ya uongozi na kukemea
ufisadi kwa nguvu moja ambapo alisema kuwa kwa sasa hakuna chama hata
kimoja kinachothubutu kusimama na kukemea ufisadi kwani nao wamekuwa
sehemu ya ufisadi huo.
Historia Zilizowekwa na ACT
Akizungumzia
historia iliyowekwa na chama hicho,Zitto alisema kuwa ACT kimeweza
kusimamisha wagombea ubunge katika majimbo 219 kati ya majimbo 265
jambo ambalo linakifanya chama hicho kuwa ni chama cha pili kwa wagombea
ubunge wengi huku cha kwanza kikiwa ni chama cha mapinduzi CCM.
Historia
nyingine ambayo chama hicho kimeiweka ni kuweza kusimamisha wagombea
ubunge wanawake wengi kuliko vyama vingine vyote nchini Tanzania ambapo
chama hicho kimesimamisha wanawake 25% sawa na wabunge 55 katika majimbo
toifauti tofauti nchini Tanzania huku kubwa ni kusimamisha mgombea
urais mwanamke.
Zitto
alitaja historia nyingine kuwa ACT wazalendo ndio chama pekee
kilichosimamisha wagombea wenye umri mdogo kuliko vyama vyote nchini
ambapo mgombea mwenye umri mdogo ana miaka 21 na mwingine akiwa na miaka
23 ambapo alisema kuwa ni ishara kuwa chama hicho kinawajali vijana.
Changamoto wanazokabiliana nazo
Akizungumzia
changamoto ambazo chama hicho kinakumbana nazo,Zitto alisema ni hujuma
mbalimbali kutoka kwa wapinzani wao ikiwemo kukatwa kwa majina kadhaa
ya wagombea wao bila sababu za msingi.
Chama
hicho kitazindua kampeni zake siku ya jumapili katika viwanja vya
zakiem mbagala Jijini Dar es salaam ambapo wanatarajia kuweka wazi
mipango na ilani ya chama hicho.
0 comments:
Chapisha Maoni