test

Jumatano, 12 Agosti 2015

TCRA yawatangazia ‘kiama’ watumiaji vibaya Mitandao


 
Meneja Mawasiliano wa TCRA, Innocent Mungy.
Watumia vibaya wa mitandao ya kijamii sasa siku zao zinahesabika  kufuatia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuanza  kutumia  sheria mpya ya makosa ya
mtandao kuanzia Septemba mosi, mwaka huu,
Mamlaka hiyo imebainisha kuwa kwa sasa Tanzania inaongoza kwa kuwa na watumiaji vibaya wengi wa mitandao ya kijamii, jambo linalosababisha taarifa za mitandao mingi kutoaminika hadi nchi za nje kutokana na kujaa uzushi, uongo, uchochezi na lugha na picha za matusi.
Kwa mujibu wa Meneja Mawasiliano wa TCRA, Innocent Mungy alikiri kuwa pamoja na kwamba mamlaka hiyo imefanya kazi kubwa ya kuelimisha jamii juu ya utumiaji sahihi wa mitandao hiyo, bado matumizi yake si mazuri hasa katika kipindi hiki cha uchaguzi na kwa watu maarufu..
Alisema kutokana na kukithiri kwa matumizi mabaya ya mitandao nchini, kwa sasa nchi nyingi haziamini tena taarifa za mitandao ya kijamii na wala hawazitumii hali inayopaswa
“TCRA tumebaini kuwa watu wengi wanatumia mitandao hii lakini hawajui hasa matumizi yake sahihi, tunashauri kabla mtu hajafungua mtandao wake kama vile blogu, ukurasa wa facebook au hata whatsApp lazima wajielimishe kwanza kuwa wanafungua kwa malengo gani, na wataitumiaji kwa manufaa yao na si vinginevyo,” amesema Mungi.
Katika hatua nyingine Rais Jakaya Kikwete ameshasaini Sheria hiyo ya Makosa ya Mtandao ya Mwaka 2015 na inatarajiwa kuanza kufanya kazi rasmi Septemba mosi, mwaka huu.
Sheria hiyo katika eneo la adhabu kwa wahalifu wa mtandao pamoja na wasambazaji wa picha za utupu na ngono, wasambazaji wa taarifa za uongo, za kibaguzi na matusi na watu wengine wanaofanya udanganyifu unaohusu kompyuta, adhabu ni kwenda jela hadi miaka 10 au kulipa faini isiyopungua Sh milioni 50.

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx

0 comments:

Chapisha Maoni