MAMLAKA ya mawasiliano nchini (TCRA) imetoa onyo kali kwa television ya Taifa TBC kwa kitendo chake cha kubagua kusoma taarifa zinazohusiana na vyama tofauti na CCM .
Hukumu hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na kamati ya maudhui ya utangazaji, katika ofisi za Mamlaka ya Mawasiliano na Kaimu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Walter Bugoya wakati wa mkutano na waandishi wa habari ambapo Bugoya amesema kamati hiyo imebaini TBC one imekiuka sheria ya utangazaji ya mwaka 2005 pamoja na sheria ya uchaguzi ya mwaka 2015 baada ya kufanya upendeleo wa vyama katika taarifa zake kwenye vipindi.
Amedai katika kipindi cha Jambo Tanzania kilichorushwa tarehe 15 mwezi huu majira ya saa 12 asubuhi hadi saa tatu,katika kipingele cha uchambuzi wa magazeti ambapo mtangazaji wa kipindi hicho alikuwa anayasoma magazeti huku akiruka kusoma habari kuu husika.
Amesema Mtangazaji huyo alipokuwa anachambua gazeti la Majira na Nipashe alidanya umma jambo ambalo amedai ni kosa.
Bugoya ametaja makosa hayo ni wakati mtangazaji huyo alipokuwa anasoma Gazati la Majira ukurasa wake wa mbele alisema habari kubwa ni “CCM yazidi waumbua wanaomfuata lowassa” wakati habari kubwa ilikuwa inasomeka hapo ni ile inayosema “Mbeya kwafurika”huku picha ya gazeti hilo likionyesha picha ya umati watu pamoja na mgombea wa Urais wa chadema Edward lowassa akihutubia.
Amesema mtangazaji huyo pia alifanya kosa jengine kama hilo pia wakati akisoma Gazeti la Nipashe ambapo alisema Habari iliyopewa uzito wa kipekee ni “Mbalawa atoa sheria ya mitandao” ambapo habari iliyopewa uzito ilikuwa ni ile ilikuwa “Mafuriko Mbeya” na sio aliyokuwa anaisoma yeye.
Amesema baada ya Kamati yake kubaini makosa hayo waliwasiliana na mkurugenzi wa TBC one Bwana Mshana ambao mkurugenzi huyo alitoa utetezi wake kwenye kamati hiyo akisema mtangazaji huyo ajafanya kosa kwakuwa alikuwa ajaridhika na taarifa zilizokuwa zimeandikwa kwenye magazeti hayo.
Sanjari na hayo Mshana alizidi jitetea akidai kuwa hata mtangazaji huyo hata asingesoma habari ile lakini picha iliyokuwa inaonekana kwenye magazeti hayo teyari mtazamaji alikuwa ashajua kwahiyo amedai haikuwa na ulazima wa kusomwa.
Bugoya amesema baada ya kusikiliza upande wa TBC one ndio wakabaini kituo hicho kilikiukaka sheria ya utangazaji ya Mwaka 2005 ambayo inavitaka vituo vyote vya utangazaji nchini kuripoti taarifa kwa kutokuwa na upendeleo wowote.
Amesema Kamati imefikia uamuzi wa kuipa onyo kali TBC one na endapo wakiendelea basi Mamlaka hiyo haitasita kuwachukulia hatua kali zaidi.
0 comments:
Chapisha Maoni