Mgombea urais kwa tiketi ya Chadema na Ukawa, Edward Lowassa jana kwa mara ya kwanza alikumbana na joto la upinzani baada ya msafara wake kushambuliwa na mabomu ya polisi.
Tukio
hilo, ambalo lilifanyika mbele ya msafara wa Lowassa, lilitokea jana
eneo la Daraja la Nduruma katika Jiji la Arusha na kusababisha umati wa
watu kutawanyika na wengine kutelekeza magari yao.
Wakati
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akimkaribisha kwenye chama hicho
wakati wa mkutano mkuu alimwambia; “Mzee huku inabidi uwe unafanya
mazoezi kidogo, kuna mabomu huku.”
Lowassa
alikumbwa na kadhia hiyo, akiwa njiani na mgombea mwenza, Juma Duni
Haji na viongozi wengine wa Ukawa, wakitokea Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), huku wakiwa wamesindikizwa na umati wa
watu na magari.
Kamanda
wa polisi mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas alisema kuwa polisi
walilazimika kupiga mabomu ya machozi ili kutawanya watu waliokuwa
wakiwarushia mawe polisi na wengine kufunga barabara.
“Kwa
hali ile, tungefanya nini? Wanatupa mawe kwa polisi na wamefunga
barabara na kuzuia magari mengine yasipite…ikumbukwe kulikuwa hakuna
kibali cha maandamano na hata kingekuja, matamko ya kuzuia maandamano
yameshatolewa,” alisema Sabas.
Katika
tukio hilo, idadi kubwa ya polisi walikuwa kwenye magari na silaha
mbalimbali ambao baadaye walianza kurusha mabomu kutawanya watu na
magari kwa eneo la daraja hilo.
Hata
hivyo, katika tukio hilo, lililotokea saa nane mchana hakuna mtu yeyote
aliyejeruhiwa na kutokana na nguvu hiyo ya polisi watu walitawanyika,
na barabara hiyo ya Arusha- Moshi ilifunguka baada ya kutopitika kwa saa
tano kuanzia saa nne asubuhi.
Akizungumza
katika mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa Tindigani, Mbunge wa jimbo
la Arusha, Godbless Lema alisema wamesikitishwa na kitendo cha polisi
kumpiga mabomu Lowassa na msafara wake.
“Tunajua
polisi wamepata maelekezo na sasa wanataka kuwatisha wananchi, lakini
tunasema leo ndiyo mwisho hatutakubali tena kunyanyaswa,” alisema Lema.
Akihutubia
mkutano huo Lowassa alitahadharisha viongozi wa polisi, kuacha kutumia
nguvu kupita kiasi, kwani anaweza kuwafikisha Mahakama ya Kimataifa ya
Jinai (ICC) iliyopo The Hague nchini Uholanzi.
Lowassa alisema alikuwa akiiamini polisi, lakini alichokiona jana cha kupigwa mabomu ni jambo baya.
Kuhusu
suala la Babu Seya aliyefungwa kifungo cha maisha gerezani alisema
atafuatiliwa kwa kutumia suala la utawala bora kwa kuangalia vyombo vya
sheria na hatua zingine zitafuatwa.
Mwenyekiti
wa Chadema, Freeman Mbowe alisema wanachama wanaojiunga sasa wana haki
sawa na mwasisi wa chama hiki Edwin Mtei mwenye kadi namba moja.
Alisema
mara baada ya wanachama wapya kujiunga, kwa kipindi cha wiki moja
nilipokea matusi mengi kuliko niliyowahi kutukanwa baada ya kupokea
wanachama wapya.
Kaimu
Mwenyekiti wa CUF, Taslima alisema kuna watu ambao wamejenga desturi ya
kuwabeza watu wanapohama vyama kwa hiari kwa kuwaita oili chafu au
makapi anavunja Katiba.
Alisema
Ibara ya 20 ya Katiba ya mwaka 1977 inasema kila mtu yeyote ambaye ni
Mtanzania, yuko huru kujiunga na mtu yeyote, chombo chochote, taasisi
yoyote atakayopenda na hatazuiliwa.
Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia alisema; “Mabomu
yamepigwa katika mkutano wa Chadema, watu wakafa Arusha, Arusha
tunayoitegemea kwa uchumi leo hii zaidi ya asilimia 19 ya pato ya taifa
linatokana na utalii, lakini leo (jana) tunaingia Arusha alipozaliwa
Lowassa tunapigwa mabomu, ukweli utatuweka huru.
0 comments:
Chapisha Maoni