Staa wa filamu Bongo, Shamsa Ford ameonesha jeuri kwa kueleza kwamba anamlea mwanaye Terry kwa mapenzi tele ili asimkumbuke baba yake, Dickson ambaye wamemwagana.
Amesema tangu wamwagane na mzazi
mwenzake, mtoto wake hajawahi kumuuliza baba yuko wapi kitendo
kinachomfanya azidishe mapenzi kwake kwani hata yeye alilelewa na mama
yake bila baba.
“Kama baba yake alikuwa akinipiga mbele yake au kuja akiwa amelewa
tilalila unafikiri mtoto atamkumbuka?
Nimelelewa na mama yangu na sikuwahi kumkumbuka baba mpaka hivi nimekuwa mtu mzima, kwa hiyo sioni shida kumlea mwanangu peke yangu, kila kukicha naongeza upendo kwake,” alisema Shamsa.
Nimelelewa na mama yangu na sikuwahi kumkumbuka baba mpaka hivi nimekuwa mtu mzima, kwa hiyo sioni shida kumlea mwanangu peke yangu, kila kukicha naongeza upendo kwake,” alisema Shamsa.
0 comments:
Chapisha Maoni