test

Jumapili, 28 Juni 2015

Android apps ambazo zitakurahisishia maisha yako ya kila siku...>>>



Instashot��- hii ni application kutoka play store ambayo inauwezo wa ku edit picha kwa kipekee. Picha unaweza iweka katika mfano wa blur kwenye background ili kusaidia picha ya mbele ionekane vizuri zaidi na kuwa na mvuto. Pia unaweza ukatumia background colours na kama zilivyo inaweza edit na video hivyo hivyo 

My Calendar��- hii ni app ingine ya bure kutoka android market ambayo ni hususani zaidi kwa wakina dada ambapo wanaweza kuhesabu siku zao katika mzunguko hususani kama mtu anataka kupata au kukwepa mimba na zaidi inawasaidia kuweza jua kama siku zao za hatari na zile ambazo =.si za hatari. 

MUHIMU⚠, hii app ni nzuri kwa wale wanawake wenye mzunguko unaoeleweka kuanzia wa siku 26 hadi wenye mzunguko wa siku 32. Kwa wale ambao mzunguko wao hautabiriki hii app haiwezi kuwa na msaada nao. 

Repost for Instagram♻ - hii app inakusaidia kuweza kutopost picha kutoka acc ingine ikiwa na caption yake, inasaidia sana pale ambapo mtu anahitaji kupost picha kama ilivyo. Achana na usumbufu wa screenshot na kupost tumia repost for instagram app. 

Islamona ��- hii ni app mahususi kwa waisalmu ambapo wanaweza kujua mda wa kuswali, muelekeo wa qibla na pia wanauwezo wa kupata Quran ya kiarabu na kiingereza ikiwa ni tafsiri. Ikifika mda wa kuswali basi adhana huita kutoka kwenye sim yako na kuweza kukukumbusha ni mda wa kuswali.

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx

0 comments:

Chapisha Maoni