Serikali
imeunda timu ya kufanya mapitio katika viwanda vya serikali
vilivyobinafsishwa ambavyo havifanyi kazi, ili virejeshwe serikalini.
Hayo
yamesemwa jana Aprili 19, 2018 Bungeni Mjini Dodoma na Waziri Mkuu
Kassim Majaliwa katika kipindi cha maswali na majibu ya hapo kwa papo.
“Serikali
imeunda timu ya kufanya mapitio kwenye viwanda vyote vya serikali
vilivyo binafsishwa ambavyo havifanyi kazi ili virejeshwe serikalini,”
alisema na kuongeza.
“Viwanda
vyote vilivyobinafsishwa vitarejeshwa serikalini na kutafutwa watu
wengine ili viendelee kufanya kazi na kutoa ajira kwa watanzania.”


0 comments:
Chapisha Maoni