Spika
wa Bunge, Job Ndugai ameitupilia mbali hoja ya Mbunge wa Ubungo, Saed
Kubenea (Chadema) kuhusiana na marekebisho ya masuala yanayohusu Tume ya
Taifa ya Uchaguzi (NEC).
Akizungumza
bungeni mjini Dodoma leo Alhamisi Aprili 12, Spika Ndugai amesema
Kubenea alileta kusudio la kuwasilisha hoja binafsi bungeni akitaka
bunge lifanye marekebisho ya masuala yanayohusiana na NEC.
“Ili
ikidhi matakwa ya mfumo wa vyama vingi hapa nchini sasa kwa kuwa Tume
hiyo ya Taifa ya Uchaguzi imeanzishwa na Katiba katika Ibara ya 74
marekebisho yote juu ya tume hiyo yanatakiwa kuletwa kwa kupitia muswada
wa marekebisho ya Katiba na si hoja binafsi ya Mbunge.
“Nafikiri
naeleweka katika ninachokisema unapoleta jambo ambalo linahusu Katiba
basi upo utaratibu wa kufuata ili iendane na marekebisho ya katiba na
siyo hoja tu ya Mbunge.
“Kwa hiyo kwa kuwa kanuni ya 58 kanuni ndogo ya kwanza ya Bunge imenipa madaraka ya kukataa hoja inayovunjwa Katiba.
“kwa
hiyo taarifa yako Mheshimiwa Kubenea naikataa kwa hiyo kajipange tena,
kama bado una nia, uje katika utaratibu unaotakiwa kama hatukukuelewa
tutatafuta muda ili tueleweshane zaidi ila sisi tumeelewa hivyo,”
amesema Spika Ndugai.


0 comments:
Chapisha Maoni