Shirika
la Ndege nchini ATCL limeondolewa katika mfumo wa malipo wa Shirika la
Kimataifa la Usafiri wa Anga IATA kutokana na kukabiliwa na madeni na
sasa limetiliana saini ya makubaliano ya miaka mitano na Kampuni ya
Ndege ya HAHN Air kuuza tiketi za Air Tanzania.
Akizungumza
na wanahabari huko Zanzibar, Mkurugenzi wa ATCL Mhandisi Ladislaus
Ernest Matindi, amesema wamelazimika kuingia kwenye makubalianao na
kampuni hiyo ili wasikose baadhi ya huduma za malipo ya tiketi.
"Tuna
madeni, sikumbuki yalifikia kiasi gani lakini ni madeni makubwa ambayo
yalilazimisha kusimamishwa uanachama au kufungiwa huduma hizi mpaka
tutakapokuwa tumelipa hayo madeni.
"Kubwa
zaidi ilikuwa ni sisi kuwa katika mfumo wa shirikisho wa mashirika ya
ndege dunia IATA ambayo ndo mfumo wa uuzaji na utawanyaji wa Tiketi.
Maana mabadilishano ya pesa au kupeleka pesa kutoka shirika moja kwenda
lingine hufanyika kwa kutumia huo mfumo wa IATA. Hii tunaanza kufanya ni
kupitia kwakweli mgongoni kwa mtu.
"Hawa
ni wanachama ambao wamepewa leseni ya kutoa huduma kwa mashirika ambayo
hayapo kwenye mfumo wa IATA. Lazima tulipe madeni yetu tuliyonayo AITA
ni mabilioni 'ni pesa nyingi kwa kweli' ili tuweze kurudi kwanza kwenye
mfumo wa kukusanya pesa" Amesema Mhandisi Ladislaus Ernest Matindi.
==>>Msikilize Hapo Chini
==>>Msikilize Hapo Chini


0 comments:
Chapisha Maoni