Skip to content
Dalili za filamu iliyowatokea jana Barcelona zilianza
kuonekana kama zinawatokea Real Madrid, hadi dakika ya 90 Juventus
tayari walikuwa mbeleni kwa mabao 3 kwa 0 katika dimba la Santiago
Bernabeu.
Shukrani kwa muamuzi Michael Oliver ambaye dakika ya 92 alitoa tuta
kwa Real Madrid ambalo liliwapa bao ambalo liliitupa nje ya michuano ya
Ulaya Juventus huku mlinda lango wao Gianluigi Buffon akipewa kadi
nyekundu.
Bao
la leo la Cristinao Ronaldo limeweka rekodu ya mchezaji mmoja kufunga
mabao mengi dhidi ya mpinzani mmoja (10) akiivunja rekodi yake mwenyewe
ya mabao 9 vs Bayern na Lionel Messi mabao 9 vs Arsenal.
Huko Allianz Arena Bayern Munich walisuluhu bao sifuri kwa sifuri na
Sevilla, matokeo haya yanawafanya Barca kufudhu kwa aggregate ya bao 2-1
baada ya ushindi walioupata Hispania wiki iliyopita.
Kwa
matokeo ya leo yanafanya nusu fainali kuwa na muwakilishi kutoka
Italia, Ujerumani, Uingereza na Hispania, hii ikiwa mara ya kwanza kwa
nusu fainali ya namna hiyo kutokea tangu mwaka 2010.
Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi
xxxxxxxxxxxxx
0 comments:
Chapisha Maoni