Serikali imetoa onyo kwa gazeti la Tanzanite kwa kosa la kuchapisha picha za utupu.
Gazeti hilo la wiki, limechapisha picha ambazo ni kinyume cha maadili za mwanadada maarufu, Mange Kimambi.
Akizungumza
jana na waandishi wa habari mjini Dodoma, Mkurugenzi wa Idara ya Habari
(MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dk. Hassan Abbas, alisema gazeti
hilo ni miongoni mwa magazeti matatu yaliyopewa onyo kwa kipindi cha
Mwezi Februari hadi mwanzoni mwa mwezi huu.
Alisema Serikali imeendelea kuchukua hatua mbalimbali kwa upande wa redio, runinga na magazeti.
“Pale ambapo maadili ya uandishi yanakiukwa au changamoto za utekelezaji wa misingi, sisi hatutasita kuchukua hatua,” alisema.
Alibainisha magazeti hayo matatu likiwamo la Tanzanite yameonywa kwa kukiuka baadhi ya misingi ya uandishi wa habari.
“Moja
ya magazeti yaliyoonywa ni pamoja na gazeti la Tanzanite, tumewaonya
kwa sababu ni mara yao ya kwanza kuchapisha picha fulani za utupu, sio
kuhusu ‘content’, ni kuhusu aina ya picha walizochapisha,” alisema.
Mkurugenzi
huyo alisema hatua hizo zimekuwa zikichukuliwa kwa magazeti mbalimbali
kwa nia njema ya kusisitiza weledi katika utendaji kazi kwenye tasnia ya
habari.
Katika
hatua nyingine, alisema katika kipindi cha Februari miongoni mwa mambo
yaliyojitokeza kimataifa ni ripoti ya hali ya rushwa na mapambano dhidi
ya ufisadi duniani ambapo Tanzania imepanda katika mapambano hayo kwa
nafasi 13 duniani.
0 comments:
Chapisha Maoni