Mbunge
wa Nzega Mjini(CCM) Hussein Bashe amefunguka na kusema wakati anaomba
kura na Mhe. Rais Dkt. Magufuli mwaka 2015 alimwambia kiongozi huyo kuwa
yeye hawezi kwenda bungeni na kuwa kati ya wale wabunge wa kusema
'Ndiyo' mzee.
Bashe amesema hayo jana alipokuwa akiongea na wananchi wa jimbo la Nzega akiwaeleza mambo mbalimbali ambayo yamefanyika katika miaka miwili jimboni hapo toka alipochaguliwa kuwa Mbunge Oktoba 25, 2015.
"Mimi
nikienda Bungeni nikisimama naposema nasema kweli kwa sababu kiapo cha
CCM kinasema 'daima nitasema kweli unafiki kwangu mwiko'
"Huo
ndio msimamo wangu na siku naomba kura na Mhe. Rais nilimwambia Rais
jukwaani kwamba Mhe. Rais mimi siendi kuwa Mbunge wa ndio mzee bali mimi
naenda kutimiza wajibu wangu na wajibu wangu ni kuisimamia, kuishauri
na kuikosoa serikali" alisema Bashe
Aidha
Mbunge huyo alisema ataendelea kubaki na msimamo wake huo wa kuisimamia
serikali labda mpaka wazee wa jimboni kwake wamshauri vinginevyo ili na
yeye akiingia akae kimya avute pesa na kutulia kimya.
"Serikali
iliyopo madarakani ni ya CCM huwezi kumuachia mtoto wa jirani kutatua
matatizo ya ndani ya nyumba yenu na huo ndiyo msimamo wangu, lakini
wazee mkisema baba eeh wewe nenda kawa mzee wa ndiyo mzee, zikija vuta
saini nenda zako mtaani basi nitafanya hivyo kwa sababu nitakula good
time kama wabunge wengine" alisisitiza Bashe
Mbali
na hilo Bashe amewaahidi wananchi wa jimbo hilo kuwa wanapoelekea mwaka
wa 2020 kuwa changamoto ya maji, umeme itakuwa historia jimboni hapo na
kusema katika suala la elimu watahakikisha wanafika kiwango ambacho
watajivunia.
0 comments:
Chapisha Maoni