Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Ally Mwalimu
amesema mpaka sasa hakuna mgonjwa wa Ebola wala anayehisiwa kuwa na
virusi vya ugonjwa huo nchini Tanzania huku Tsh. bilion 1.5 zikiwa
zimetumika kuukabili ugonjwa huo
Ummy
amebainisha hayo leo wakati alipokuwa anazungumza na wanahabari jijini
Dar es Salaam na kusema wananchi wasiwe na hofu ila wanapaswa kuchukua
tahadhari huku akisisitiza kuwa wameweka kifaa maalum 'register' ambacho
kitawalazimu wasafiri wote kujaza wakiwa wanakwenda katika nchi ya DRC
na pindi wakiwa wanatoka huko kuingia nchini.
"Hadi
sasa hakuna mgonjwa hata mmoja wa Ebola wala mwenye virusi Tanzania,
tumechukua tahadhari katika mikoa yote inayopakana na nchi ya Congo DRC.
Wasafiri wote wanaotoka DRC wakifika Tanzania lazima waandikishwe
kimaalum ili kufuatiliwe kama huko alikotoka hali ikoje na kama hana
virusi nyemelezi. Tunawaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza
katika kuwapima wasafiri wote kwenye mipaka yetu na Congo DRC" alisema Ummy.
Aidha,
Ummy amesema serikali imeagiza mashine nne za nyongeza kutoka nje ya
nchi ili kuongeza nguvu ya upimaji wa virusi vya ugonjwa huo.
0 comments:
Chapisha Maoni