test

Jumatano, 24 Mei 2017

Rais Magufuli Atapokea Taarifa ya Kamati Maalum ya kuchunguza mchanga Saa Tatu Asubuhi Hii


Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, inawataarifu wananchi wote kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo  tarehe 24 Mei, 2017 atapokea Taarifa ya Kamati Maalum aliyoiunda kuchunguza mchanga ulio katika makontena ya mchanga wa madini (Makinikia) yaliyopo katika maeneo mbalimbali hapa nchini Tanzania.

Tukio la kupokea taarifa hiyo litahudhuriwa na viongozi mbalimbali na kurushwa moja kwa moja kupitia vituo vya habari vya redio, televisheni na tovuti rasmi ya Ikulu ambayo ni www.ikulu.go.tz

Wananchi mnakaribishwa kutazama na kusikiliza matangazo hayo yatakayorushwa hewani kuanzia saa 3.30 Asubuhi kutoka Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx

0 comments:

Chapisha Maoni