Mvua
imesababisha barabara kuu ya Mwanza -Bukoba kukatika eneo la Kemondo,
hivyo magari ya abiria na mizigo kuzunguka Kyetema kupitia Katerero
kutokea Muleba.
Barabara
hiyo ilikatika jana (Ijumaa) saa 11:00 alfajiri kutokana na mvua
iliyonyesha usiku kucha na kusababisha maji kujaa kwenye karavati.
Kutokana
na hali hiyo wananchi na hasa wafanyabiashara wa eneo la Kemondo
wameshindwa kuendelea na shughuli zao kwa kukosa mawasiliano.
Meneja
wa Wakala wa Barabara (Tanroads) Mkoa wa Kagera, Andrew Kasamwa amesema
watumiaji wa barabara hiyo wanatumia njia mbadala kwa kupita Katerero
mzunguko wa umbali wa takriban kilomita 10.