Sakata
la masheikh wa Uamusho walioshtakiwa kwa tuhuma za ugaidi, limeibuka
bungeni jana baada ya Mbunge wa Konde, Khatib Said Haji (CUF) kuhoji ni
nchi gani ambayo haina tishio la kigaidi inaweza kuwa na mlundukano wa
watu wenye makosa hayo kwenye magereza.
“Hapa
katika jibu nimeambiwa siku 60 zinatosha kutoa ushahidi na kwamba, kama
ushahidi haukupatikana, watuhumiwa waachiwe. Lakini masheikh wa Uamsho
wana miaka minne sasa wapo katika magereza na ushahidi umeshindwa
kupatikana,” alisema Khatib.
Alihoji iwapo watuhumiwa hao wanawekwa mahabusu kwa
kuwa wana kesi ya kujibu, au kwa amri ya viongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ).
“Waziri wa vikosi vya SMZ Zanzibar na Makamu wa Rais Zanzibar wamewahi kunukuliwa wakisema kwamba waliwaleta masheikh Tanzania ili wanyee ndoo katika magereza ya Tanzania Bara.” Alisema Khatib Said Haji
“Waziri wa vikosi vya SMZ Zanzibar na Makamu wa Rais Zanzibar wamewahi kunukuliwa wakisema kwamba waliwaleta masheikh Tanzania ili wanyee ndoo katika magereza ya Tanzania Bara.” Alisema Khatib Said Haji
Akijibu
swali hilo, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Yusuph Masauni
alisema kesi za watuhumiwa hao zipo mahakamani na kwa taratibu
hawaruhusiwi kujibu hoja kortini.
Hali
hiyo ilisababisha baadhi ya wabunge kuguna bungeni hali iliyomfanya
Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe kuongezea majibu ya
swali hilo.
Dk
Mwakyembe alisema ni kweli kwamba sheria inataka mahakama kama
upelelezi haujakamilika ndani ya siku 60, mtuhumiwa kuachiwa huru,
lakini Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa (RCO) anaweza kupeleka maombi
mahakamani ya kuongezwa siku.
Alisema
baada ya hapo suala linakuwa chini ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) na
kwamba, kulingana na uzito wa shtaka anaweza kuomba kuongeza muda.
“Suala la ugaidi si dogo ni la kimtandao na kuutambua huo mtandao si suala dogo,” alisema Dk Mwakyembe