Katika
kuelekea Kilele cha Maadhimisho ya Sherehe ya Kutimiza Miaka 40 ya
Chama Cha Mapinduzi, Wanaccm Wilaya ya Longido Kata ya Namanga Jana
tar. 04/02/2017 Wamekutana na kufanya Shughuli za Jamii ikiwemo kufanya
Usafi wa Mazingira Katika Hospitali ya Serikali iliyopo Kata ya Namanga.
Aidha Juzi pia waliwatembelea watoto Yatima Wanaolelewa na kituo Cha Masai Foundation Kata ya Namanga Chini ya Msimamizi wake Mama Kabati.
Waliweza
kutoa msaada wa vitu mbalimbali vya kuwasaidia watoto hao ikiwemo
chakula. Wanaccm hao kupitia Katibu wa CCM Wilaya ya Longido Mama
Esuphati Naikara alisema CCM inatambua Changamoto mbalimbali
zinazowakabili Watoto Yatima Wanaolelewa na Vituo Vya Watoto Yatima
hivyo wameamua Kwa Umoja weo kuwasaidia wanyonge hao.
"Leo
katika Kumbukumbu tunawakumbuka Waasisi wa CCM Hayati Baba wa Taifa
Mwl. Julius Kambarage Nyerere, Hayati Mzee Aboud Jumbe ( Mungu azidi
kuwarehemu na Kupumzisha Roho zao kwa Amani ) Kwa Mchango wao Mkubwa ktk
Kuunda CCM Imara & Madhubuti ambayo Leo inaongozwa na Mzee wa Hapa
Kazi tu Mwenyekiti CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mh. Dkt. John Pombe Magufuli ambaye ni Mchapa Kazi hodari
kwelikweli, Mwenye Mapenzi mema na Nchi yetu, Mwenye kutetea Wanyonge,
Mwenye nia ya dhati ya Kuwatumikia Watanzania..Watanzania & Wanaccm
kwa Ujumla tunampongeza sana na Kumuombea kwa Mungu azidi kumlinda ili
akatuongoze vyema."Alisema Katibu wa CCM Wilaya ya Longido Mama Esuphati Naikara
Katika Hatua nyingine Mjumbe wa Baraza Kuu UVCCM Mkoa wa Arusha Ndg.Robert PJN Kaseko amekabidhi Kiasi Cha Tsh. 100,000/= Kwa
Katibu wa CCM Kata ya Namanga Ndg. Moody S.Jumaa Kwa ajili ya Chama
hicho Cha Mapinduzi ili Kuwawezesha Viongozi Kutimiza Majukumu yao
vizuri ya Ujenzi wa Chama. Fedha imepokelewa Mbele ya Katibu Msaidizi
wa CCM Wilaya ya Longido Ndg.Laraposh Laizer na Wanaccm.
CCM Hoyeeeeeeeeeeee. Kidumu Chama Cha Mapinduzi.
Wana
CCM Wilaya ya Longido Kata ya Namanga wakifanya Usafi wa Mazingira
Katika Hospitali ya Serikali iliyopo Kata ya Namanga Jana.
Mjumbe
Baraza Kuu UVCCM Mkoa wa Arusha Ndg.Robert PJN Kaseko akikabidhi Pesa
Kiasi Cha Tsh. 100,000/= Kwa ajili ya CCM ili Kuwawezesha Viongozi
Kutimiza Majukumu yao vizuri ya Ujenzi wa Chama.
Wanaccm
Wilaya ya Longido Wakiwa katika picha ya Pamoja na watoto Yatima
Wanaolelewa na kituo Cha Maasai Foundation Kata ya Namanga. Wana CCM Wilaya ya Longido Kata ya Namanga wakiwa katika Picha ya Pamoja Baada ya Kufanya Usafi wa Mazingira Katika Hospitali ya Serikali iliyopo Kata ya Namanga Wilayani Longido.