Waziri
Mkuu wa zamani, Edward Lowassa amevunja ukimya kuhusu mgogoro wa
uhalali wa Uenyekiti wa Profesa Ibrahim Lipumba anayetambuliwa na Ofisi
ya Msajili wa Vyama vya Siasa unaoendelea ndani ya Chama Cha Wananchi
(CUF) ambao umekuwa ukihusishwa naye tangu awali.
Lowassa
ambaye alitajwa na Profesa Lipumba kuwa chanzo cha yeye kujiuzulu kabla
ya kurejea tena miezi 9 baadae kutengua uamuzi wake, amesema kuwa shida
za chama hicho ni shida za vyama vyote vinavyounda Ukawa.
Mwanasiasa
huyo mkongwe na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, ametumia ukurasa wake
wa Facebook kueleza jinsi ambavyo Ukawa inalibeba tatizo la mgogoro wa
CUF.
“CUF
ni wenzetu katika Ukawa. Shida zao ni shida zetu, vita vyao ni vita
vyetu, kushindwa kwao ni kushindwa kwetu, ushindi wao ni ushindi wetu,” aliandika Lowassa.
Kauli
hiyo ya Lowassa imekuja miezi michache baada viongozi wa Ukawa kueleza
msimamo wao kuwa hawamtambui Profesa Ibrahim Lipumba kama Mwenyekiti wa
CUF na kwamba wataendelea kushirikiana na Katibu Mkuu wa Chama hicho,
Maalim Seif Sharif Hamad.
Naye Profesa Lipumba amekuwa akieleza kuwa hayuko tayari kuona Chadema au Lowassa wanakinunua chama hicho.
Hivi karibuni, Ukawa wameweka msimamo wao kuwa watawasimamisha wagombea wa pamoja katika uchaguzi mdogo utakaofanyika mwakani.
Hata
hivyo, kumekuwa na changamoto baada ya pande mbili zinazovutana ndani
ya CUF kila mmoja kutangaza kuwasimamisha wagombea wake huku Tume ya
Taifa ya Uchaguzi ikiweka msimamo kuwa ili iwatambue wagombea wa chama
hicho ni lazima fomu zao zisainiwe na pande mbili zinazovutana.
Miezi
michache kabla ya kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana, Profesa
Lipumba alionekana akimtambulisha Lowassa mbele ya waandishi wabari na
kujibu maswali mengi yaliyoelekezwa kwake lakini siku chache baadae
alitangaza kujiuzulu akida moyo wake unamsuta hawezi kumuunga mkono
mwanasiasa huyo.