Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa ilmeeleza kuwa Rais Magufuli amesaini sheria hiyo jana tarehe 16 Novemba 2016 na kuwapongeza wadau wote kwa kufanikisha kutungwa kwake.
Novemba 4 mwaka huu Rais Magufuli katika mkutano wake na wahariri wa vyombo vya habari nchini alisema kuwa mara tu sheria hiyo itakapofikishwa kwake ataisaini mara moja.
Rais Magufuli alisema hayo huku kukiwa na malalamiko kutoka kwa wadau wa habari nchini wakiomba muda kupitia sheria hiyo na kutoa maoni yao