Waziri
wa Nishati na Madini wa Tanzania, Profesa Sospeter Muhongo na Waziri wa
Nishati na Maendeleo ya Madini wa Uganda, Mhandisi Irene Muloni
wametembelea eneo la Chongoleani mkoani Tanga ambako kutajengwa hifadhi
ya mafuta pamoja na gati itakayotumika kupakia mafuta kwenye Meli
mbalimbali ili kusafirishwa.
Mafuta
hayo yatapakiwa kwenye Meli hizo baada ya kusafirishwa na Bomba kutoka
Hoima nchini Uganda kwa ajili ya kusafirishwa nje ya nchi.
Akiwa
katika eneo hilo Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini wa Uganda
aliwaeleza wananchi wa eneo hilo kuwa nchi ya Uganda inaishukuru
Tanzania kwa kukubali Bomba hilo lipite katika ardhi ya Tanzania suala
ambalo litakuwa na faida mbalimbali kwa Wananchi ikiwemo mabadiliko ya
kiuchumi.
Alisema
kuwa lengo ni kuona kuwa mradi huwa huo unaanza kazi mwaka 2020 na
ndiyo maagizo ambayo Marais wa nchi mbili wameyatoa kwa watendaji
wanaosimamia Mradi huo wa Bomba la Mafuta.
Mhandisi
Muloni alitumia fursa hiyo kuwaasa wananchi kujiandaa kikamilifu kwa
fursa za kiuchumi kwani watekelezaji wa mradi watahitaji huduma
mbalimbali kama za chakula, malazi na usafiri hivyo kupitia utoaji wa
huduma hizo wananchi nao watapata kipato.
Pia
alizishukuru Sekta Binafsi za Uganda na Tanzania kwa kuwa tayari
kushirikiana na Serikali ili kuhakikisha kuwa mradi huo unafanikiwa
akitolea mfano kampuni ya GBP ya Tanzania ambayo imeonesha nia ya
kununua hisa katika kampuni itakayoanzishwa kwa ajili ya usimamizi wa
Bomba hilo la Mafuta.
Pia
alizishukuru kampuni za TULLOW ya Uingereza, CNOOC ya China na TOTAL ya
Ufaransa kwa kuamua kutekeleza mradi huo ambao utawezesha jumla ya
mapipa laki mbili ya mafuta kusafirishwa kwa siku kupitia Bomba hilo la
Mafuta lenye urefu wa kilomita 1443.
Kwa
upande Profesa Muhongo alisema kuwa Bomba hilo pia litatumika
kusafirisha mafuta kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) baada
ya nchi hiyo kugundua mafuta.
Alisema
kuwa Waziri kutoka DRC anayesimamia Nishati hiyo amefika nchini ili
kufanya mazungumzo na Tanzania juu ya kutekeleza suala hilo ambapo
inakadiriwa kuwa nchi hiyo itakuwa ikisafirisha mapipa 30,000 hadi
100,000 kwa siku kupitia Bomba hilo la Mafuta.
Alisema
kuwa Gati hiyo ya Chongoleani ina uwezo wa kupakua mafuta kwa muda wa
mwaka mzima kutokana na kutokumbwa na mawimbi makubwa ya bahari ambayo
hupeleka shughuli hiyo kusuasua.
“
Ndugu zangu shughuli ya upakiaji wa mafuta katika Bandari hii
itafanyika kwa muda wa mwaka mzima kwani Bandari hii haina mawimbi
makubwa yatakayozuia shughuli hii kufanyika, na ndiyo moja ya vigezo
vilivyotumika katika kuchagua Bandari hii kupokea mafuta kutoka
Uganda,”alisemaProfesa Muhongo.
Kwa
upande wa Wananchi, baadhi ya Wananchi hao walisema kuwa wamepokea
mradi huo kwa matumaini makubwa ambapo wamesema kuwa wana imani kuwa
mara mradi utakapoanza wataweza kupata huduma mbalimbali ikiwemo Elimu,
Afya, Miundombinu ya barabara n.k.
Naye
Profesa Muhongo aliwaasa wananchi hao kuwa na subira wakati Serikali
ikiwa inafanya mipango mbalimbali ili kuhakikisha kuwa mradi huo
unafanyika kwa ufanisi.