test

Jumanne, 6 Septemba 2016

Wajanja wanaoendelea kutumia simu feki waonywa

Waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, amesema wananchi wanaoendelea kutumia simu feki ama zisizokidhi viwango vya kulinda afya ya watumiaji ama zenye namba tambulishi bandia, wanaweza kudhurika na matumizi yake.

mobile-phones
Amesema hayo Jumanne hii katika kipindi cha maswali na majibu bungeni wakati akijibu swali la mhemishiwa Bahati Aliabeid mbunge wa Mahonda, lililohoji, “Je, serikali inafikiria nini kuhusu kutoa elimu kwa umma kuhusu simu feki?”
“Wananchi ambao wanaendelea kutumia simu feki ama zisizokidhi viwango vya kulinda afya ya watumiaji ama zenye namba tambulishi bandia wanaweza kudhurika na matumizi yake kwani hazikutengenezwa kwa kupitia mfumo unaothibiti simu hizo kutokuwa na kemikali hatari zinazoweza kudhuru binadamu na mazingira kwa mfano Zebaki na kemikali zinginezo,” alisisitiza Profesa Mbawara.
“Pia Mbarawa alisema, “Kabla na baada ya kuzima simu feki, serikali imekuwa ikielimisha umma kuhusu tahadhari ya kutotumia simu hizo ili kuepuka madhara ambayo yanaweza kutokea kwa kutumia simu hizo zisizokidhi matakwa ya kulinda afya ya watumiaji.”
Kwa upande mwingine Profesa Mbawara, alisema serikali inaendelea kutoa elimu kwa umma kuhusu wananchi kujiepusha na matumizi ya simu hizo ikiwa ni pamoja na kuzikusanya na kuzichoma moto kwa mujibu wa utaratibu uliopo.Waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, amesema wananchi wanaoendelea kutumia simu feki ama zisizokidhi viwango vya kulinda afya ya watumiaji ama zenye namba tambulishi bandia, wanaweza kudhurika na matumizi yake.
mobile-phones
Amesema hayo Jumanne hii katika kipindi cha maswali na majibu bungeni wakati akijibu swali la mhemishiwa Bahati Aliabeid mbunge wa Mahonda, lililohoji, “Je, serikali inafikiria nini kuhusu kutoa elimu kwa umma kuhusu simu feki?”
“Wananchi ambao wanaendelea kutumia simu feki ama zisizokidhi viwango vya kulinda afya ya watumiaji ama zenye namba tambulishi bandia wanaweza kudhurika na matumizi yake kwani hazikutengenezwa kwa kupitia mfumo unaothibiti simu hizo kutokuwa na kemikali hatari zinazoweza kudhuru binadamu na mazingira kwa mfano Zebaki na kemikali zinginezo,” alisisitiza Profesa Mbawara.
“Pia Mbarawa alisema, “Kabla na baada ya kuzima simu feki, serikali imekuwa ikielimisha umma kuhusu tahadhari ya kutotumia simu hizo ili kuepuka madhara ambayo yanaweza kutokea kwa kutumia simu hizo zisizokidhi matakwa ya kulinda afya ya watumiaji.”
Kwa upande mwingine Profesa Mbawara, alisema serikali inaendelea kutoa elimu kwa umma kuhusu wananchi kujiepusha na matumizi ya simu hizo ikiwa ni pamoja na kuzikusanya na kuzichoma moto kwa mujibu wa utaratibu uliopo.

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx