Rais Magufuli ameagiza mkataba wa kampuni ya Ticts inayopakia na kuondosha mizigo bandarini ufanyiwe marekebisho ili kulinufaisha Taifa kutokana na oparesheni zake bandarini.
Vilevile ameiagiza Mamlaka ya Bandari Tanzania(TPA) inunue mashine nne za kukagulia mizigo inayoingia bandarini hapo.
Ameitaka TPA na waziri husika kufunga floor meters ndani ya miezi minne.
Pia TPA ijenge bandari kavu Mlandizi na kutozitumia binafsi zilizopo kwakuwa zinatumika kukwepa kodi.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa imeeleza hayo alipokutana na wafanyakazi wa bandari.