Wakati akihutubia wananchi waliokuwa wakazi wa Magomeni Kota, leo jijini Dar es salaam, Rais John Magufuli amesema kuwa Serikali yake inaendelea kufanya juhudi za kuboresha miundombinu ya jiji hilo ili kubadili muonekano wake na kuonekana kama majiji ya nchi zilizoendelea.
"Lengo langu ni kuifanya Dar es salaam inakuwa jiji la kisasa hata mgeni akiikanyaga asione tofauti na majiji mengine duniani "alisema
" MaDC, Katibu Tarafa, Mameya na Wakurugenzi hakikisheni mnaifanya Dar es salaam kuwa jiji la kisasa na la biashara ili wananchi wafanye biashara na watajirike "
Rais John Magufuli amesema kuwa Serikali iko katika mazungumzo na serikali ya Uingereza ya kujenga barabara za juu' Fly Over 'eneo la Ubungo.
" Ukiacha Fly Over ya Tazara, tutajenga nyingine ubungo na kwamba tuko katika mazungumzo na serikali ya Uingereza ili kupata fedha za kujenga barabara hiyo "alisema
Amesema kwa kutambua umuhimu wa mabadiliko ya jiji la Dar es salaam kumepelekea kuteua viongozi wachapakazi ili kutimiza azma yake.
" DSM inahitaji mabadiliko ya kweli kwa kumleta mtu atakayeweza kutatua changamoto zilizopo, ndio maana nilimchagua Makonda, Hapi na wengine kwa kuwa niliwaamini wataweza pambana na changamoto zilizopo".

