Mrema ameyasema hayo wakati akizungumza katika kipindi cha Power Breakfast cha Clouds Fm na kusema kuwa wanatakiwa kufanya siasa kama anayoifanya yeye ya kuwa mpinzani mstaarabu ambaye anaunga mkono kazi zinazofanywa na Rais Magufuli.
“Mimi ni mpinzani mstaarabu, upinzani wa kijinga siutaki kama wewe ni mpinzani wa kweli inatakiwa ukae bungeni ili kutoa matatizo ya watanzania lakini sasa wao wanatoka ningekuwa mimi nisingetoka, niwashauri tu wakae wafanye kazi,” alisema Mrema.
Aidha Mrema aliwaonya Chadema kuacha kupanga kufanya maandamano ya UKUTA kwani rais wa sasa ana nia ya dhati kuwafanyia kazi watanzania na kama wamekosa kazi ya kufanya waende shambani kulima au kusaidia kutatua tatizo la madawati.
“Rais ameshasema apewe muda kuleta maendeleo kwa watanzania na yeye ndiyo mwenye majeshi kama wamepanga kufanya maandamano wasidhani kitawakuta kama kilichonikuta mimi mwaka 1995, rais anataka tu kazi kama hawana ya kufanya waende mashambani kulima au wakatafute madawati,” alisema Mrema.