Mchungaji
wa Kanisa la Maombezi (GRC) la Ubungo jijini Dar es Salaam, Anthony
Lusekelo maarufu ‘Mzee wa Upako’ amesema kitendo cha viongozi wa CCM
kulitaja zaidi jina la Edward Lowassa katika Mkutano Mkuu Maalumu wa
chama hicho ni ishara kuwa Waziri Mkuu huyo wa zamani ni tishio.
“Nani! Lowassa…. jina lake kutajwa sana katika vikao vya CCM. Hiyo inaashiria kuwa ni mtu tishio. Ndiyo ni tishio,” alisema Lusekelo jana katika mkutano wake na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam........
Lusekelo
ambaye hivi karibuni, Rais John Magufuli alishiriki ibada katika kanisa
lake, alimzungumzia Lowassa baada ya kuulizwa swali juu ya mtazamo wake
kuhusu Mkutano Maalumu wa CCM ambao jina la mgombea huyo wa urais
kupitia Chadema na Ukawa lilitajwa na makada wengi wa chama hicho
tawala.
Alisema
hilo lilidhihirika hata katika mchakato wa CCM kupata mgombea wake wa
urais, kutokana na Lowassa kuungwa mkono kwa kiasi kikubwa.
Alisema
kitendo cha Waziri Mkuu huyo wa zamani kuzua mjadala katika Mkutano
Mkuu wa chama hicho tawala sambamba na wimbi la makada wanaohama vyama
vyao, si mambo yanayopaswa kuwa mjadala kwa sababu uchaguzi ulishapita.
Huku
akisema: “Sizungumzi haya kwa ajili ya kujipendekeza, sihitaji ukuu wa
wilaya,” Lusekelo aliwataka viongozi kukataa kuendeleza uhasama wa
kisiasa na chuki kwa maelezo kuwa mwaka huu uwe maalumu kuzika tofauti
hizo, kufanya kazi kulijenga Taifa na kuhubiri amani na umoja.
Katika
mkutano huo, Lusekelo alipongeza kuimarika kwa vyama vya upinzani
akaponda mvutano ulioibuka bungeni akisema kukosa uzoefu kwa Naibu
Spika, Dk Tulia Ackson kulichangia huku akiunga mkono kauli ya Rais
kuzuia shughuli za siasa na kubainisha jinsi Rasimu ya Katiba ya Tume ya
Jaji Joseph Warioba, ilivyopendekeza kupunguzwa kwa madaraka ya Rais.
Jumamosi
iliyopita, katika Mkutano Mkuu wa CCM mjini Dodoma, uliomalizika kwa
Rais Magufuli kuchaguliwa kuwa mwenyekiti, mzimu wa Lowassa ulitawala
kutokana na kila aliyepewa nafasi ya kuzungumza ama kumtaja kwa jina au
kwa mafumbo.
Mwenyekiti
wa CCM aliyemaliza muda wake, Jakaya Kikwete ndiye aliyeanza
kuzungumzia hali ya mchakato wa chama hicho kupata mgombea wake wa
urais, kuwa ulikuwa mgumu na majaribu makubwa na kwamba wazee walifanya kazi kunusuru hali hiyo.
Katika
mchakato huo, CCM ilikata jina la Lowassa katika hatua za awali, jambo
lililosababisha kiongozi huyo kuhama na kundi la wanaCCM na kujiunga na
Chadema ambayo ilimteua kuwa mgombea wake wa urais.
Hata
hivyo, katika mkutano wake wa jana, Lusekelo alisema katika mchakato wa
chama hicho tawala kupata mgombea wake wa urais kulikuwa na watu wenye
majina makubwa, akiwamo Lowassa na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje,
Bernard Membe.
“Niliwaambia
CCM, Membe huwezi kumpuuza, Lowassa naye huwezi kumpuuza maana wanataka
madaraka na kwa vyovyote lazima mtapata mtikisiko. Nikawaomba
waahirishe suala la kupata Katiba Mpya maana wasingelimaliza na muda
ulikuwa mfupi,” alisema na kuongeza: “Kama mwaka huu hautatumika kutibu majeraha yaliyotokea huko nyuma, tutaharibikiwa sana.”
Alisema
mchakato wowote wa uchaguzi na kura ya maoni ndani ya vyama huacha
mpasuko na watu hutumia dini na ukabila kubaguana, hivyo lazima baada ya
uchaguzi mambo hayo yamalizwe.
“Tunapaswa
kukumbuka kuwa wote ni Watanzania tusahau uchaguzi. Sasa ni wakati wa
kuijenga nchi. Amani inatengenezwa, na Mungu huwapa hekima maana kujenga
ni kazi na kubomoa ni rahisi, huu ni mwaka wa uponyaji na kurejesha
Taifa pamoja,” alisema Lusekelo.
Alisema
kuanza kubagua watu kwa sababu walitoka CCM kwenda Chadema au kutoka
Chadema kwenda chama tawala si jambo sahihi huku akitolea mfano mataifa
yaliyovurugika kwa kuendekeza siasa za chuki na uhasama.
Yaliyotokea bungeni
Akizungumza
yaliyotokea bungeni na kusababisha wabunge wa Ukawa kususia vikao vya
Bunge vilivyoongozwa na Dk Tulia, Lusekelo alisema Mtanzania anayejua
historia ya nchi yake hawezi kufumbia macho suala hilo.
“Binafsi
nawalaumu waliotoka (wabunge wa upinzani) na waliobaki (wabunge wa
CCM). Kushindana si kuzuri. Mbatia (James Mbunge wa Vunjo na Mwenyekiti
wa NCCR-Mageuzi) na wenzake wanapaswa kujua kuwa naibu spika ni mchanga
katika siasa waende naye taratibu maana kapewa ubunge tu na kuwa naibu
spika,” alisema.
Huku akiponda uamuzi wa Serikali kufuta urushwaji wa matangazo ya moja kwa moja ya Bunge alisema: “Nashangaa
wazee kama Salim (Ahmed Salim – Waziri Mkuu mstaafu), Pinda (Mizengo –
Waziri Mkuu mstaafu) na Warioba. Sijui walishindwa nini kukaa na wabunge
hawa ili kumaliza tofauti zao.”
Alisema si jambo jema kuongoza nchi kwa mabavu na kusisitiza kuwa hata uhuru ulipatikana kwa mazungumzo.
Mchungaji huyo aliusifu utawala wa Rais Magufuli kuwa una kasi kubwa na kwamba licha ya wananchi kulia ukata, watacheka baada ya mwaka mmoja huku akiwananga wanaomponda Kikwete kuwa hawajui mazuri aliyoyafanya.
Mchungaji huyo aliusifu utawala wa Rais Magufuli kuwa una kasi kubwa na kwamba licha ya wananchi kulia ukata, watacheka baada ya mwaka mmoja huku akiwananga wanaomponda Kikwete kuwa hawajui mazuri aliyoyafanya.
Awapongeza wapinzani
Akizungumzia nguvu ya vyama vya upinzani, Lusekelo alisema ushindani wa kisiasa umekuwa mkubwa kutokana na kuimarika kwa upinzani: “Chadema ya sasa si ile ya miaka ya 1990. Wanaongoza miji mikubwa na ukiona chama kina wabunge 40 usikipuuze. Hata nguvu ya mfalme ni watu.”
Akizungumzia nguvu ya vyama vya upinzani, Lusekelo alisema ushindani wa kisiasa umekuwa mkubwa kutokana na kuimarika kwa upinzani: “Chadema ya sasa si ile ya miaka ya 1990. Wanaongoza miji mikubwa na ukiona chama kina wabunge 40 usikipuuze. Hata nguvu ya mfalme ni watu.”
Mikutano ya siasa
Kuhusu kauli ya Rais kusitisha shughuli za siasa hadi mwaka 2020, alisema jambo hilo linaweza kuonekana baya lakini lina unafuu mkubwa, kwamba Kenya wamelifanya na kufanikiwa kumaliza tofauti za kisiasa.
Kuhusu kauli ya Rais kusitisha shughuli za siasa hadi mwaka 2020, alisema jambo hilo linaweza kuonekana baya lakini lina unafuu mkubwa, kwamba Kenya wamelifanya na kufanikiwa kumaliza tofauti za kisiasa.
“Hivi
watu 10,000 wakiandamana na kusema Magufuli aliiba kura itakuwaje? Tuna
askari wa kuwazuia! Nadhani wanasiasa wafanye kazi ya utawala katika
vyama vyao. Tutulie kwanza tutibu majeraha. Hakuna jambo baya kama
kuwaongoza watu wenye njaa maana hawana la kupoteza,” alisema.
Hata
hivyo, Lusekelo alisema Rasimu ya Katiba ilipendekeza Rais kupunguziwa
madaraka na huenda madaraka makubwa aliyonayo Rais yakawa sababu ya nchi
kuendelea kuwa na amani.
“Kenya
kuzuia maandamano ni ngumu sana lakini hapa kwetu hadi Zitto
(Kabwe-Kiongozi wa ACT-Wazalendo) alizuiwa kufanya mkutano wa ndani.
Kwetu rais ana madaraka makubwa sana,” alisema huku akiwataka polisi kutekeleza wajibu wao vyema, wakikumbuka kuwa nao ni binadamu.