Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete jioni ya jana,
ameungana na mamia ya waombolezaji katika mazishi ya mwanasiasa mkongwe
wa Tanzania, Peter Kisumo ambaye amezikwa nyumbani kwake katika Kijiji
cha Ngujini, Wilaya ya Mwanza, Mkoa wa Kilimanjaro.
Akitokea
Dodoma ambako amekuwa anaongoza vikao vya Chama cha Mapinduzi (CCM),
Rais Kikwete akifuatana na Mama Salma Kikwete, alijiunga na mamia ya
waombolezaji wakati wa salamu zilizokuwa zinatolewa na watu mbali mbali
katika Kanisa ya Usharika wa Kilindu la Kanisa la Kiinjili la Kilutheri
Tanzania (KKKT).
Mzee
Peter Abdallah Kisumo ambaye alizaliwa Agosti Mosi, mwaka 1935 katika
Wilaya ya Pare, Mkoa wa Kilimanjaro aliaga dunia Jumapili ya Agosti 2,
mwaka huu, akiwa na umri wa miaka 80.
Wakati
wa kutoa salamu, Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Asha Rose Migiro
alitoa kwa niaba ya Serikali na kwa niaba ya Rais Kikwete, na Mzee
David Cleopa Msuya alitoa shukrani kwa niaba ya familia ya Mzee Kisumo.
Mara
baada ya kumalizika kwa salamu hizo kwenye Kanisa la Usharika wa
Kilindu, Rais Kikwete aliongozana na mwili wa marehemu ambao ulikuwa
umepambwa kwa bendera ya CCM kwenda Kijijini Ngujini kwa mazishi. Mwili
wa Marehemu Kisumo uliteremshwa kaburini kiasi cha saa 11:15 jioni.
Mzee
Kisumo ambaye alianza maisha yake ya kazi kama Bwana Shamba wa Serikali
kabla ya kuingia katika uongozi wa vyama vya wafanyakazi alipata pia
kuwa Waziri wa Serikali katika vipindi mbali mbali na Mkuu wa Mikoa ya
Kilimanjaro (mara mbili), Singida, Pwani, Dar es Salaam na Mwanza.
Rais Kikwete aliondoka Kilimanjaro mara tu baada ya mzishi hayo kurejea Dodoma
0 comments:
Chapisha Maoni