WATU 15 wameuawa kwa kukatwa mapanga katika matukio tofauti mkoani Geita kwa imani za ushirikina.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Joseph
Konyo alisema matukio hayo ya mauaji yametokea katika miezi mine
kuanzia Januari hadi Aprili mwaka huu.
Konyo
alisema mauaji hayo yametokana na imani potofu za ushirikina na
wahusika wakubwa wa matukio hayo ni waganga wa kienyeji wanaopiga ramli
chonganishi.
“Kwa
mwaka huu mpaka hivi sasa tulikumbwa na matukio 15 ya mauji
yaliyotokana na imani za ushirikina ambako katika wilaya tano kulikuwa
na wastani wa watu watatu ambao waliuawa, lakini tunashukuru matukio
haya tumepungua kwa sababu ya operesheni ya kuwasaka waganga,” alisema Konyo.
Wakati
huohuo, Kamanda Konyo amethibitisha kuwa mtu mmoja, Lyoba Juma (23),
mkazi wa Kijiji cha Milwa Butiama amefariki dunia kwa kugongwa na gari
ya Land Cruiser mali ya Mgodi wa GGM iliyokuwa likiendeshwa na Yusuph
Hashibeli.
Alisema
tukio hilo lilitokea ndani ya mgodi wa dhahabu wa GGM eneo la WD1
wakati Juma na vijana wenzake walipokwenda kupora mawe yanayodhaniwa
kuwa na dhahabu.
Kamanda
alisema walinzi waliokuwa katika doria waliwafukuza na yeye aliteleza
katika kifusi na kubiringika mpaka barabarani ndipo tairi za nyuma ya
gari hiyo ilipomkanyaga kichwani.
0 comments:
Chapisha Maoni