KAMA
mti mbichi unatenda haya, itakuwaje kwa mti mkavu?! Ndivyo inavyoweza
kutafsiriwa kwa Katibu Mtendaji wa Idara ya Mawasiliano wa Baraza la
Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania (Tanzania Episcopal Conference,
TEC), Padri Anatoly Salawa kufuatia kunaswa kichakani akiwa na mrembo.
Kiongozi
huyo wa dini alinaswa hivi karibuni majira ya saa 8: 02 usiku akiwa
ndani ya gari aina ya Toyota RAV 4 lenye nambari ya usajili T 674 ADA
kwenye kichaka kilichopo maeneo ya viwanda na gereji za magari makubwa,
Kurasini jijini Dar.
Huku
mvua kubwa ikinyesha na baridi ikipuliza vilivyo achilia mbali baadhi
ya maeneo ya jiji kutotulia kwa mafuriko na foleni, waandishi wetu
walipigiwa simu na mlinzi mmoja wa Kimasai wa kwenye gereji hizo na
kunyetisha juu ya gari lililosimama karibu na eneo lao la lindo huku
likinesanesa.
Mlinzi
huyo alieleza kuwa yeye na wenzake walilichunguza kwa makini gari hilo
na kuona kuwa ndani yake kulikuwa na watu wawili wa jinsi tofauti lakini
walishindwa kujua wazi kilichokuwa kikiendelea.
Mlinzi
huyo alisema kuwa mara kwa mara gari kama hilo limekuwa likifika hapo
majira ya usiku wa manane hivyo kuwafanya kuingiwa na shaka.
Waandishi
walifika eneo la tukio ndani ya muda mfupi na kuwakuta polisi nao
wakiwasili kisha kuchukua kwanza maelezo kwa walinzi hao bila kuwashtua
wahusika kwenye gari.
Baada
ya mahojiano na walinzi hao, walilifuata gari hilo na kulipekua ambapo
hawakuamini macho yao baada ya kumkuta mtu mzima huyo katika gari hilo
akiwa na mrembo aliyekuwa mtupu.
Huku mvua ikiendelea kumwagika, padri huyo alionekana akiwa ametaharuki ndani ya gari asijue la kufanya.
Mara
baada ya kuwanasa wawili hao, padri alijitetea kwa kusema kuwa, alikuwa
ameingiliwa na wahuni katika starehe zake hivyo aliingia kwenye gari na
kutimua na mrembo wake.
Jana
padri huyo alitafutwa tena ili kama ana la ziada la kusema alitoe
lakini simu yake ya kiganjani iliita bila kupokelewa na baadaye ikazimwa
kabisa.
Baada
ya muda simu hiyo iliwashwa tena na ndipo alipotumiwa ujumbe mfupi wa
simu ya mkononi (SMS) . Hata hivyo, SMS hiyo haikujibiwa.
Padri Anatoly akijistili baada ya tukio hilo.
Baada
ya SMS hiyo, padri huyo aliendelea kupigiwa simu lakini bado iliita
bila kupokelewa ndipo akatumiwa ujumbe mwingine uliosomeka hivi; ‘mkuu
tumepata tukio lako ukiwa kichakani ndani ya gari usiku na mrembo akiwa
mtupu. Wewe unalizungumziaje tukio hili? Kwa maana nyingine
unajiteteaje? Tunaomba maelezo yako’.
Kama ilivyokuwa kwa ujumbe wa kwanza, nao huo haukujibiwa.
Chanzo: Gazeti la Ijumaa/Gpl
0 comments:
Chapisha Maoni