KAMATI Kuu ya Chama cha ACT-Wazalendo, ilikuwa na kikao chake cha kawaida cha siku mbili kilichokaa tarehe, 23 na 24 mwezi huu na kuongozwa na Mwenyekiti wa Taifa, Anna Mghwira, pia kilihudhuriwa na kiongozi wa Chama Zitto Zuberi Kabwe.
Agenda za vikao hivyo vya siku mbili zilikuwa ni
- Uteuzi wa nafasi mbali mbali za kiutendaji ndani ya chama
- Operesheni majimaji
- Ratiba ya Uchaguzi mkuu na Ngome za Chama
UTEUZI
Baada ya agenda hizo kujadiliwa kwa kina wajumbe wa kamati kuu waliafikiana kuwateua wanachama wafuatao
1. MANAIBU KATIBU WAKUU BARA NA ZANZIBAR
Kwa upande wa Naibu katibu mkuu bara kamati kuu imemteua MNEC
Msafiri, Abrahaman Mtemelwa ambaye ni mwanasiasa mzoefu katika siasa za
Tanzania na miongoni mwa vijana wa kwanza kusimamia siasa za upinzani
nchini.
Mtemelwa ameshika nafasi mbali mbali za uongozi katika vyama vya
siasa nchini, ambapo alishakuwa Mwenyekiti wa Kwanza wa vijana wa
NCCR-Mageuzi,na baadae kuwa mkurugenzi Habari na uenezi na mkurugenzi wa
Kampeni na Uchaguzi wa Chadema kazi alizoziifanya kwa mafanikio makubwa
kabla ya kujiunga na ACT-Wazalendo.
Pia kamati kuu ya ACT –Wazalendo, imemteua Juma Said Sanani, kuwa Naibu katibu Mkuu Zanzibar
Juma Sanani, alishawahi kushika nafasi mbali mbali za kiuongozi katika vyama vya CUF na ADC kabla ya kujiunga na ACT-Wazalendo
Mwaka 1992 alijiunga na Chama cha CUF kabla chama hicho hakijapata usajili wa kudumu akiwa ni mwanachama wa kawaida
1993-1999 alikuwa mkurugenzi wa fedha wilaya ya mjini Unguja
1999-2009,Sanani alichaguliwa kuwa mjumbe wa mkutano mkuu wa Taifa wa
CUF akitumikia nafasi ya afisa mipango na Uchaguzi katika Idara ya
Mipango na Uchaguzi.
2009-2012 Sanani alikuwa mkurugenzi wa Uchaguzi CUF Taifa
2012 alijiunga na Chama cha ADC na kushikilia nafasi ya Naibu katibu
mkuu Zanzibar mpaka alipojiunga na Chama cha ACT-Wazalendo machi 2015.
2. MAKATIBU WA KAMATI MBALIMBALI
Kamati kuu imemteua Peter Mwambuja kuwa katibu wa Fedha na Rasilimali
Mwambuja ni msomi wa ngazi ya CPA katika masuala ya mahesabu,
aliyewahi kufanya kazi katika maeneo mbali mbali ya nchi akiwa mhasibu
Wengine walioteuliwa na nafasi zao katika mabano ni
Habibu Mchange
(Mipango na Mikakati),
Richard Sabini
(Mawasiliano na Uenezi)
Mohamed Masaga (Kampeni na Uchaguzi)
Deus Chembo (Katiba na Sheria)
Venance Msebo (Mambo ya Nje)
Gibson Kachinjwe (Katibu kamati ya Maadili na Uadilifu)
3. NAFASI YA WENYEVITI
Kamati kuu imemteua Estomih Mallah kuwa mwenyekiti wa Kamati ya Fedha
na Rasilimali na Mwanasheria wakili Msomi Albert Msando, ameteuliwa
kuwa Mwenyekiti wa kamati ya Katiba na Sheria
WAJUMBE WA KAMATI KUU
Kamati kuu imewateua Mzee Japhari Kasisiko na Hamad Mussa Yusuph kuwa wajumbe wa Kamati kuu
WASHAURI WA CHAMA
Kamati kuu kwa nafasi yake imewateua Profesa Kitilla Mkumbo na Tery Bermunda(mama Tery) kuwa washauri wa Chama.
OPERESHENI MAJIMAJI
Kamati kuu imeazimia kufanya operesheni ya ujenzi wa Chama katika
majimbo 59 kwenye mikoa 19, operesheni iliyopewa jina la Maji Maji na
kwamba operesheni hii itaanza mapema iwezekanavyo
Lengo la operesheni maji maji litakuwa ni kueneza na kujenga chama na
kukagua uhai wake chama kazi itakayofanyika kwa siku 12 kwa timu kumi
za kazi kujigawa katika maeneo mbali mbali
RATIBA YA UCHAGUZI
Kamati kuu imekasimu kwa sekretariti ya Chama shughuli ya uandaaji wa
ratiba na taratibu za uchaguzi kuanzia uchukuaji wa fomu na
kuzirejesha, malipo ya ada ya fomu za wagombea kwa nafasi mbali mbali za
kuanzia udiwani, Ubunge na Urais kwa nchi nzima
Pia kamati kuu ya ACT-Wazalendo, iliiagiza sekretariti ya Chama
kuandaa utaratibu mzima uchaguzi wa Ngome za vijana, wanawake na wazee
na kwamba uchaguzi wa ngome hizo ufanyike kabla ya ratiba ya uchaguzi
mkuu.
Imetolewa na
Abdallah Khamis.
Afisa Habari ACT Wazalendo
26/05/2015
0777008686
0 comments:
Chapisha Maoni