test

Alhamisi, 31 Mei 2018

Zitto atangaza ushirikiano na Chadema Jimbo la Buyungu


Image result for zitto na mbowe
Jana Jumatano Mei 30, 2018, Zitto kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii ameeleza kuwa yeye na mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe wamekubaliana kuwa watashawishi kuwepo na ushirikiano wa vyama vya upinzani katika uchaguzi huo.
 
Uchaguzi wa Buyungu utafanyika baadaye mwaka huu baada ya aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Kasuku Bilago kufariki dunia Mei 26, 2018.
 
“Kwa heshima ya mwalimu Bilago mimi na Mbowe tumekubaliana kuwa tutashawishi kuwepo na democratic front (ushirikiano wa kidemokrasia) katika Jimbo la Buyungu,”amesema Zitto.
 
“Ama ACT itaunga mkono mgombea wa Chadema au Chadema itaunga mkono mgombea wa ACT Wazalendo. Tunataka kuweka mgombea mmoja anayekubalika na wananchi wa Buyungu na kufanya kampeni kwa pamoja mpaka ushindi.”
 
Amesema huo ni mwanzo wa harakati za kuwa na ushirikiano imara wa kidemokrasia dhidi ya ukandamizaji wa demokrasia nchini na hali mbaya ya maisha ya wananchi.
 
“Umoja wa zaidi ya vyama vya siasa ukihusisha vyama vya wafanyakazi, vyama vya wakulima, vyama vya wafanyabiashara na wananchi wengine,” amesisitiza mbunge huyo.

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx

0 comments:

Chapisha Maoni