Naibu
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt.
Suzan Kolimba amesema Suala la Mauaji ya Kimbari sio jambo la kufikirika
kwani limeshatokea katika nchi za ukanda wa Maziwa Makuu na ndio maana
Serikali katika nchi hizo zimekuwa zikiandaa mikakati mbalimbali ili
kuhakikisha tukio hilo linakuwa historia..
Dkt.
Kolimba amesema hayo alipokuwa akifungua semina ya Wabunge ambao ni
wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge za Katiba na Sheria na Mambo ya
Nje, Ulinzi na Usalama ambapo alimwakilisha Waziri wa Katiba na Sheria
Prof. Palamagamba Kabudi.
“Mauaji
ya kimbari sio jambo la kufikirika, limeshawahi tokea katika nchi zetu,
ndio maana kumekuwa na mikakati mbalimbali ili kuhakikisha mauaji kama
hayo yanakuwa historia, tunataka mauaji haya yawe historia kwa nchi zetu
na yasije jirudia tena,” alisema mhe. Kolimba
Alisema
kwamba nchi za maziwa makuu kwa sasa zinatakiwa kuongelea maendeleo na
mashirikiano na sio vita au ubaguzi wa aina yoyote ile.
Alisema
viongozi wanatakiwa kujua kuwa wameshilikilia hatma za watanzania
mikononi mwao na hivyo hawana budi kuweka mbele utu, uzalendo na utaifa
dhidi ya tashwishi za kisiasa kwa mustakabali mzuri wa wananchi.
Mhe.
Kolimba alitumia nafasi hiyo kuipongeza Tanzania na Kamati ya Kitaifa
ya mauaji ya Kimbari kwa kuwa ni moja ya nchi zilizotajwa na Umoja wa
Mataifa kuwa zinafanya vizuri katika eneo hilo.
Kikao
hicho kinachifanyika mjini Dodoma kinalenga kuwapitisha Wabunge ambao
ni wajumbe wa Kamati hizo juu ya Mkataba wa Kuzuia mauaji ya kimbari kwa
nchi za Maziwa Makuu wa mwaka 2006 ili kuwapatia uelewa kuhusu kuzuia
mauaji ya kimbari, uhalifu wa kivita na ubaguzi dhidi ya binadamu.
Tanzania
pamoja na nchi nyingine 12 za Maziwa Makuu walitia saini kuridhia
utekelezaji wa mkataba huo. Nchi hizo ni pamoja na Kenya,
Uganda,Rwanda,Burundi, Congo DRC, Sudani Kusini, Sudani,Zambia,Angola,
Jamhuri ya Afrika ya Kati na Jamhuri ya Congo.
Semina
hiyo ya wabunge imeandaliwa na Kamati ya Kitaifa ya kuzuia mauaji ya
Kimbari nchini kwa kushirikiana na Ofisi ya Mshauri Maalum wa Umoja wa
Mataifa wa kuzuia mauaji ya kimbari ya New York Marekani.


0 comments:
Chapisha Maoni