Mbunge
wa jimbo la Kawe (CHADEMA) Halima Mdee amefunguka na kumuomba Jaji Mkuu
Prof. Ibrahim Hamis Juma kufuatilia mwenendo wa kesi za kisiasa nchini
na kudai kuwa baadhi ya mahakimu wamekuwa wakipindisha mambo kwa sababu
za kisiasa.
Halima
Mdee amesema hayo wakati akiongea na kituo cha EATV na kusema kuwa Jaji
Mkuu anaposema wanasiasa wasiingilie Mahakama hivyo na yeye anapaswa
kusimama na kuhakikisha kuwa Mahakimu wakitenda haki na kukemea wale
ambao kwa makusudi wamekuwa wakipindisha haki za watu.
"Ni
zaidi ya wiki sasa Mhe. Sugu yupo ndani lakini amenyimwa dhamana kwa
kosa ambalo linadhaminika kisheria na kiutaratibu kwa mujibu wa sheria
zetu kama kosa linadhaminika ni wajibu wa polisi kutoa dhamana na polisi
wakikushikilia ndani ya zile saa 48 wakikupeleka mahakamani ni jukumu
la Mahakama kufanya hivyo sasa suala la Sugu limeenda Mahakamani ambapo
huo ndiyo muhimili pekee ambao tunautegemea .
"Sasa
unapokwenda Mahakamani sehemu pekee ambayo unaitegemea kupata haki
halafu unaona hiyo haki haipatikani kwa makusudi kabisa hivyo Jaji Mkuu
na yeye anapaswa kuyatambua haya na kuwakemea baadhi ya Mahakimu ambao
wanafanya vitu kama hivi" alisema Mdee
Mbali
na hilo Halima Mdee amedai kuwa kuna tetesi za kutaka kumfunga Mbunge
wa Mbeya Mjini Mhe. Joseph Mbilinyi “Sugu' kama ambavyo alifungwa Mbunge
wa Kilombero, Peter Lijualikali.
0 comments:
Chapisha Maoni