Leo
July 5 2017 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ililazimika kuhamia kwa
muda katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete(JKCI) iliyopo Hospitali
ya Taifa ya Muhimbili, na kumsomea mashtaka saba ya uhujumu uchumi,
mfanyabiashara Maarufu Yusufu Manji na wenzake watatu. Hatua hiyo
imefikiwa baada ya Manji kushindwa kufika mahakamani kwa ajili ya
kusomewa mashtaka kutokana na kulazwa katika taasisi hiyo.
Akisoma hati ya mashtaka
mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi, jopo la Mawakili Waandamizi
wa serikali wakiongozwa na Mutalemwa Kishenyi, Nassoro Katuga na
Tulumanywa Majigo.
Washtakiwa
hao wanadaiwa walijipatia bidhaa isivyo halali mnamo Juni 30,2017
katika maeneo ya Chang’ombe A Temeke Jijini Dar es Salaam walikutwa na
askari polisi wakiwa na mabunda 35 ya vitambaa vinavyotumika kutengeneza
sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) zenye thamani ya Sh milioni
192.5 ambazo zilipatikana isivyo halali.
Katika
shitaka jingine inadaiwa washtakiwa hao walikutwa na mhuri wa serikali
wa JWTZ isivyo halali Juni mnamo 30,2017 ambao umeandikwa” Mkuu wa
Kikosi 121 kikosi cha JWTZ” bila ya kuwa na uhalali na kwamba kitendo
hicho kinahatarisha uchumi na Usalama wa nchi.
Washtakiwa
hao hawakutakiwa kujibu mashtaka hao Kwa sababu makosa hayo hapo chini
ya uhujumu uchumi na Usalama wa taifa. Hata hivyo, upande wa mashtaka
uliwasilisha hati ya pingamizi la dhamana kutokana Kwa Mkurugenzi wa
Mashtaka ya Umma(DPP).
Katika
hati hiyo, DPP alidai,ikiwa washtakiwa hao watapewa dhamana wanaweza
kuhatarisha Usalama na maslahi ya nchi na Kwa mujibu wa sheria kulingana
na shtaka la 1 na 2, mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haina mamlaka ya
kisheria ya kutoa dhamana Kwa washtakiwa hao.
Hata
hivyo, hoja hiyo ilipingwa na upande wa utetezi ukiongozwa na Wakili
Hudson Ndusyepo alidai kuwa mashtaka hayo yanaiondolea mahakama
kuwafikiria wateja wake dhamana.
Kutokana
na kuwepo Kwa mabishani ya kisheria,Hakimu Shaidi alisema masuala
yanapaswa kuongelewa kwenye mahakama yenye mamlaka kisheria Kwa sababu
DPP hajaipa mamlaka ya kisheria ya mahakama ya Kisutu kusikiliza maombi
ya dhamana. Kutokana na hali hiyo, kesi hiyo imeahirishwa hadi Julai
19,mwaka huu Kwa ajili ya kutajwa.
0 comments:
Chapisha Maoni