December 03 2016 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli, amefanya uteuzi wa Mabalozi 15 ili kujaza nafasi
zilizo wazi katika Balozi za Tanzania zilizopo katika nchi mbalimbali.
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza
kuwa Mabalozi hao wameteuliwa kwa ajili ya kuiwakilisha Tanzania katika
vituo vifuatavyo;
- Beijing – China
- Paris – Ufaransa
- Brussels – Makao Makuu ya Jumuiya ya Nchi za Ulaya
- Muscat – Oman
- Rome – Italy
- New Delhi – India
- Pretoria – Afrika ya Kusini
- Nairobi – Kenya
- Brasilia – Brazil
- Maputo – Msumbiji
- Kinshasa – Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
- Kampala – Uganda
- Abuja – Nigeria
- Moroni – Comoro
- Geneva – Umoja wa Mataifa
Aidha, Mhe. Rais Magufuli amefanya uteuzi wa Mabalozi 6 kwa
ajili ya kuiwakilisha Tanzania katika Balozi mpya 6 ambazo zitafunguliwa
hivi karibuni katika nchi za Algeria, Israel, Korea ya Kusini, Sudan,
Qatar na Uturuki.
Orodha kamili ya Mabalozi walioteuliwa ni kama ifuatavyo;
- Balozi Mbelwa Brighton Kairuki
- Balozi Samuel W. Shelukindo
- Balozi Joseph E. Sokoine
- Balozi Silima K. Haji
- Balozi Abdallah Kilima
- Balozi Baraka Luvanda
- Balozi Dkt. James Alex Msekela
- Bw. Sylvester Mwakinyuke Ambokile
- Pindi Chana
- Dkt. Emmanuel J. Nchimbi
- Rajab Omari Luhwavi
- Lut. Jenerali (Mstaafu) Paul Ignace Mella
- Grace Mgovano
- Mohamed Said Bakari
- Job Masima
- Omar Yusuf Mzee
- Matilda S. Masuka
- Fatma M. Rajab
- Sylvester M. Mabumba
- Prof. Elizabeth Kiondo
- George Madafa (Uteuzi wake ulishatangazwa)
Vituo vya kazi vya mabalozi hawa 21 vitatangazwa baadaye.
Mabalozi wote waliobaki katika vituo ambavyo si kati ya vituo hivi 15
vilivyotajwa wataendelea na nafasi zao za uwakilishi wa Tanzania katika
vituo walivyopo.
Katika hatua nyingine, Rais Magufuli amemhamisha
Balozi Modest Jonathan Mero kutoka kituo chake cha sasa cha Geneva,
kwenda Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa (New York) ambako atakuwa
Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa.
Balozi
Modest Jonathan Mero anachukua nafasi ya Mhe. Balozi Tuvako M. Manongi
ambaye atastaafu ifikapo tarehe 06 Desemba, 2016.
Katika hatua nyingine,
Mhe. Rais Magufuli amemteua Bibi Grace A. Martin kuwa Balozi na
Mkurugenzi wa Itifaki (Chief of Protocal) – Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki kuanzia leo tarehe 03 Desemba, 2016.
Kabla
ya uteuzi huo Grace A. Martin alikuwa akikaimu nafasi hiyo. Wakati huo
huo, Rais Magufuli amemteua Balozi Peter Kallaghe kuwa Afisa Mwandamizi
Mwelekezi – Mambo ya Nje katika Chuo cha Taifa cha Ulinzi (National
Defence College)
Kabla ya uteuzi huo, Balozi Peter Kallaghe alikuwa
Balozi wa Tanzania nchini Uingereza hadi mwanzoni mwa mwaka huu 2016.

