test

Jumanne, 18 Oktoba 2016

Mahakama yamwamuru Mbowe alipe deni la NHC


Hukumu hiyo imetolewa Jumanne hii na jaji mfawidhi wa mahakama hiyo,Sivangilwa Mwangezi ambaye amesema kuwa taratibu zote zilifuatwa kuondoa vitu katika jengo hilo.
Hata hivyo alisema katika hukumu hiyo hakuna aliyevunjiwa haki yake ya msingi kutokana na kufuatwa kwa sheria dhidi ya madai ya shirika la nyumba NHC kwa Mbowe Hotels.
Wakili wa upande wa Mbowe Hotels,John Malya amesema wamepokea hukumu na kuomba nakala ili kuifanyia kazi na pia alisema kuwa nakala wakiipata wanaweza wakaamua katika kukata rufaa.
Na kwa upande wa wakili wa NHC, Aliko Mwamnenge amesema kutokana na hukumu hiyo ya Mbowe Hotels wanadaiwa shilingi bilioni 1.7 na NHC na amesema vitu haviwezi kurudishwa mpaka pale mlalamikiwa atakapolipa deni lake kwa NHC.

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx